Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge, Owen Mwandumbya akihutubia alipokuwa akizundua rasmi Bunge la Vijana la mwaka 2016, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, mjini Dodoma jana. Mkutano huo ni wa tatu toka kuanzishwa kwa Bunge la Vijana chini ya mradi Legislatures Support Project(LSP).
Spika wa Bunge la Vijana, Regnald Massawe (kushoto) kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha akimuapisha Stella Wadson-kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii kuwa Naibu Spika wa Bunge hilo baada ya kuanza kwa mkutano wa tatu wa Bunge la Vijana la mwaka 2016, mjini Dodoma. Picha na Ofisi ya Bunge
Spika wa Bunge la Vijana, Regnald Massawe (kulia) kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha akila kiapo mbele ya Katibu wa bunge hilo, Agness Mwamanda kutoka Chuo cha Mzumbe baada ya kuanza kwa mkutano wa tatu wa Bunge la Vijana la mwaka 2016, mjini Dodoma. Picha na Ofisi ya Bunge
Wabunge wa Bunge la Vijana la mwaka 2016, kutoka Vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juuu wakila kiapo cha utii baada ya kuanza kwa mkutano wa tatu wa bunge hilo, mjini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge, Owen Mwandumbya katika picha ya pamoja baada ya kuzundua rasmi Bunge la Vijana la mwaka 2016, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, mjini Dodoma jana. Mkutano huo ni wa tatu toka kuanzishwa kwa Bunge la Vijana chini ya mradi Legislatures Support Project(LSP).







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...