Serikali imepongeza taasisi isiyo ya Kiserikali ya Makumbusho Urithi Tanga kwa jitihada nzuri walizofanya za kuandaa makumbusho itakayo hifadhi utamaduni wa wakazi wa Mkoa wa Tanga.

Pongezi hizo zimetolewa leo jijini Tanga na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo alipotembelea Makumbusho hayo ya Urithi Tanga alipokuwa katika ziara yake ya kikazi mkoani hapo iliyolenga kujua uendeshwaji wa shughuli za kisekta.

“Kazi hii ya ukusanyaji wa taarifa mbalimbali za wakazi wa Tanga kuanzia ngazi ya Makabila yote saba ya Mkoa wa Tanga,Mila na Desturi zao, pamoja na kuhimiza ukarabati majengo ya kale kweli mnahitaji pongezi kwa uzalendo huo”,

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akitazama baadhi ya picha zenye historia zilizohifadhiwa katika Makumbusho ya Urithi wa Tanga (kushoto) ni Mkurugenzi wa Makumbusho hayo Mhandisi Raymond Mhando akitoa maelezo ya picha hizo.

“Serikali ya China iliahidi kusaidia kujenga Majumba ya Makumbusho kwa nchi za Afrika hivyo andikeni barua ya Wizarani kuwa ajili ya kuendeleza makumbusho haya halafu tutaiwasilisha Ubalozi wa China”.alisema Naibu Waziri Wambura,

Kwa upande Mkurugenzi wa Makumbusho ya Urithi Tanga Mhandisi Godwin Mhando alisema lengo la kuanzisha makumbusho hayo ilikuwa ni kutaka kutunza historia ya Mkoa wa Tanga pamoja na kulinda kuhifadhi Mila na Desturi za watu wa Tanga kwa ajili ya vizazi vijavyo kwani Mkoa huo unahistoria kubwa katika nchi.

“Makumbusho haya ya Urithi Tanga siyo kwa maslahi binafsi bali kwa wanatanga wote na tumeamua kufanya uhifadhi huu kwa kuwa tumeona ipo haja ya kuhifadhi historia Mkoa wetu.”alisema Mhandisi Mhando.

Jengo la Makumbusho ya Urithi wa Tanga linalohifadhi Utamaduni wa wakazi wa Tanga pamoja na historia jiji la Tanga Mkoani hapo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa alisema ofisi yake itajitahidi kushirikiana na viongozi wa makumbusho hayo kwa kuhakikisha inafikia malengo iliyojiwekea kwa maslahi ya wakazi wa Tanga pamoja na Watanzania wote kwa ujumla.

Aidha Mkurugenzi huyo wa makumbusho aliendelea kusema kupitia ofisi hiyo wamekuwa wakipanga siku ambayo hufanya maonesho ya shughuli za kiutamaduni kama matibabu ya kiasili,kuwepo kwa vyakula vya asili hii ikiwa ni siku ya maadhimisho ya kuenzi utamaduni wa wakazi wa Tanga.

Hata hivyo kila Mtanzania ametakiwa kujali asili yake pamoja utamaduni wake na pia kuenzi kwani ni urithi mkubwa kwa vizazi vijavyo.imeandikwa na Anitha Jonas – MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...