Mgeni
Rasmi katika semina ya kitaalam iliyofanyika Jijini Dar es salaam leo
ambaye ni Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam , Alhaji Mussa Salum,
akitoa mada katika semina maalum ya wataalam mbalimbali iliyokuwa na
lengo la kujadili kwa pamoja swala la siku ya QUDS Duniani ambayo n i
siku maalum ya kuwakumbuka na kupaza sauti kuwatetea wananchi wa Taifa
la palestina ambao wamekuwa wakipata mateso makubwa kutoka katika Taifa
la israel siku ambayo iliazimishwa Jana Duniani kote huku watu
mbalimbali wakifanya matembezi ya kuonyesha kuguswa na swala hilo.
Akizngumza
katika semina hiyo ya Wataalam iliyofanyika Jijini Dar es salaam katika
ukumbi wa Karemjee Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa
Salum amesema kuwa swala la maisha ya wananchi wa Nchi ya Palestina ni
swala la wanadamu wote bila kujali itikadi za kidini hivyo ni Jukumu ya
kila mwanadamu kusimama kuwatetea wananchi ambao wanaporwa ardhi yao na
Taifa la Israel..
Ameongeza
kuwa katika kuazimisha siku ya QUDS Duniani ni siku sio ya wapalestina
pekee bali ni siku ya kuazimishwa na dunia nzima kwakuwa mateso
wanayopata wanadamu wenzetu ni makubwa na hayavumiliki hata kidogo.
Balozi
wa palestina nchini Tanzania HAZEEM SHABAT akizungumza katika semina
hiyo ambapo amesema kuwa hadi kufikia sasa watu zaidi ya 48488
wamepoteza mahali pa kuishi tangu mwaka 1967 jambo ambalo limekuwa
hatari sana kwa wanadamu hao ambao hawana hatia.
Balozi huyo
amesema kuwa Ni wakati sasa wa mataifa yanayopenda haki likiwemo Taifa
la Tanzania kuinuka kwa pamoja na kuungana ili kupigania Haki ya nchi ya
palestina ili waweze kuachiwa Ardhi yao ambayo imekuwa inadhulumiwa na
Taifa la Israel na kusababisha madhara makubwa likiwemo la maafa na
unyanyasaji mkubwa kwenye ardhi yao.
Balozi
wa Jamhuri ya watu wa IRAN nchini Tanzania MEHDI AGHA JAFAI akitoa mada
katika semina hiyo maalumu ya wataalam mbalimbali iliyofanyika kwa
lengo la kujadili kwa undani mgogoro wa nchi hizo mbili ikiwa ni jana tu
dunia imeadhimisha siku ya QUDS Duniani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...