Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa Stamiko Deusdedith Magala,akizugumzana na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya wameanzisha vituo sita vya kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo katika mikoa sita,leo jijini Dr es Salaam.


Wanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa Stamiko wakionesha jinsi walivyoimarisha usalama na uokoaji migodi,leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

Akizungumza katika maonyesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba wakati wakionesha jinsi namna usalama na uokoaji unavyofanyika katika mgodi wa Biharamulo, Kaimu Mkurugenzi wa Stamiko Deusdedith Magala, alisema kuwa vituo hivyo vitakuwa katika mikoa sita kwa ajili ya kutoa mafunzo ya usalama kwa wachimbaji wadogo.

Alivitaja vituo hivyo kuwa ni Mkoa wa Kagera, Mara, Mbeya Singida Mwanza na Geita ambavyo watakuwa wanatoa elimu ya usalama kwa wachimbaji wadogo kuepuka ajali migodini.

Hata hivyo aliwataka wachimbaji wadogo kuhakikisha wanafika katika vituo vya stamiko vilivyopo karibu kupatiwa elimu jinsi ya kuepuka ajali zinazotokea migodini mara kwa mara. "Suala la usalama na uokoaji katika Migodi inatakiwa kupewa kipaumbile ili kuepuka ajali za mara kwa mara kwa wachimbaji wadogo wakielimika ajali za migodini zitaepukika,"alisema Magala.

Kwa Upande wake Mjiolojia Mkuu wa Mgodi wa Biharamulo Ayoubb Nyenzi aliyemwakilisha meneja wa mgodi wa dhahabu wa Biharamulo, Amesema Tanzania ina wataalamu wazuri wa kuchimba madini hivyo ni vyema serikali ikawapa nafasi zaidi ili kuhakikisha rasilimali hiyo inaleta manufaa zaidi hapa nchini.

Nyenzi alisema mgodi huo unashirikiana kwa karibu na jamii inayozunguka mgodi ambapo wameweza kutoa madawati 2000 kwa shule pamoja na ujenzi wa shule ya sekondari. Aliendelea kusema wameweza kufanya biashara na wananchi wanaozunguka eneo hilo kwa kuwapatia elimu ya kilimo cha mboga mboga na matunda ambapo wanauzia mgodi na wameweza kujipati milioni 2000.

Naye Mrakibu wa usalama afya na uokoaji Mgodini Fotunatus Japi, alisema suala la usalama lazima lizingatiwe hususani kwa wachimbaji wadogo na wakubwa. Alisema katika mgodi wao wa Biharamulo wamekuwa wakizingatia suala la usalama kwa kuwa iwapo majanga yakitokea kunaathiri soko la dhahabu inayotoa mgodini hapo.

Hata hivyo alisema wanatumia juhudi zote kuhakikisha hakuna majanga na pale yanapotokea kunakuwepo na uokoaji wa uhakika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...