Makamu wa Rais wa Huduma wa Shirika la Ndege la Etihad, Sajida Ismail, Makamu wa Rais wa Uhusiano wa shirika hilo, Calum Laming akipokea tuzo za Skytrax World Airline ya World Best First Class Airline, World’s Best First Class Onboard Catering na World’s Best First Class Airline Seat
Shirika la ndege la Etihad limetunukiwa tuzo tatu za ubora wa juu kwenye madaraja pia tuzo ya ubora kwenye huduma za vyakula pia tuzo ya ubora kwenye malazi kutoka Skytrax Worldairline Awards, zilizotangazwa NCHINI uingereza.
Tuzo hizo za World Airline ni za kimataifa na huhusisha mashirika ya ndege yanayofanya vizuri katika sekta ya usafiri wa anga. Mshindi huchaguliwa kwa kura kutokana na mchakato ambao huchukua miezi 10 kukamilika kwake huku ikujumuisha wasafiri takribani milioni 18 kutoka katika nchi zaidi ya 100 ulimwenguni.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...