Na Daudi Manongi
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa sikukuu za
Eid al Fitr na Sabasaba zilisababisha ukosefu wa nishati ya Petroli Mkoa wa Mtwara na
kuathiri wa baadhi ya shughuli za maendeleo.
Hatua hii ilitokana na wamiliki wengi wa ‘deport’ za mafuta kufunga kwa ajili ya
kushiriki sikukuu hizo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja Mawasiliano na Uhusiano (EWURA) Bw.Titus
Kaguo wakati wa mahojiano na Idara ya Habari(MAELEZO) wakati akitoa ufafanuzi
juu ya uhaba wa tatizo hilo katika Mkoa wa Mtwara lililoripotiwa na baadhi ya vyombo
vya habari.
Alisema kuwa hivi sasa hali ya upatikanaji wa nishati hiyo imerejea kwani vituo vingi
vimeanza kuuza nishati hiyo baada ya sikukuu hizo kumalizika.
Bw.Kaguo alisema kuwa kutokana na biashara hiyo kuendeshwa na watu binafsi na
wahusika hao kushiriki sikukuu hiyo ilisababisha kusimama kwa shuguli hiyo, hatua
ilivifanya baadhi ya vituo kukosa nishati ya mafuta na kushindwa kufanya kazi katika
kipindi hiki cha sikukuu.
Aidha amewahakikishia wananchi kuwa kwa sasa nishati ya Petroli na Dizeli ipo kwa
wingi kwani kwa siku ya jumanne dizeli lita milioni (5) tano ziliuzwa ukilinganisha na
matumizi ya nchini ya siku ambayo ni lita milioni 4.8 na kwa Petroli lita zilizouzwa ni
milioni 3.6 ukilinganisha na matumizi ya nchi nzima ya petroli ya lita milioni 2.8. kwa
siku.
Aliongeza kuwa toka jumanne vituo kama Lake Oil,Tsn na Central belt vimeendelea
kutoa huduma kama kawaida kwa wananchi wa Mkoa wa Mtwara.
Mji wa Mtwara siku ya Jumatano ulikumbwa na uhaba wa mafuta ya Petroli na hivyo
kufanya wakazi wa mji huo kununua nishati hiyo kwa bei ya ulanguzi toka lita shilingi
1950 hadi kufikia shilingi 2500 kwa lita jambo liloathiri shughuli za maendeleo ya
wananchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...