Mkurugenzi Mtendaji wa Azam TV, Tido Mhando(Katikati) akizungumza na waandishi wa habari  jijijini Dar es Salaam leo hawapo pichani wakati wa kuingia makubaliano ya kununua haki za matangazo ya kurusha laivu mashindano ya ligi kuu ya Vodacom kwa miaka 5 kuanzia msimu wa 2016 hadi 2020. Kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi ya TFF, Boniface Wambura na kushoto ni  Meneja wa Vipindi wa Azam Tv, Yahaya Mohamed.
Meneja wa Vipindi wa Azam Tv, Yahaya Mohamed akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azam TV, Tido Mhando na kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi ya TFF, Boniface Wambura.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini (TFF) umeingia mkataba wenye thamani ya Bilioni 23 kwa miaka mitano na kampuni ya Azam Media kwa kununua haki ya kurusha matangazo ya mpira wa ligu kuu Vodacom kuanzia msimu wa 2016.

 Katika mkataba huo kila timu katika itavuka milioni 42 kwenye kila robo ya msimu na kwenye robo ya mwisho timu itapata fedha kulingana na nafasi yake kwenye msimamo wa ligi. 

Mkurugenzi mtendaji wa Azam Media, Tido Mhando amesema kuwa mkataba huo umeboreshwa na kila timu sasa inatakiwa ifanye vizuri ili mwisho wa msimu iweze kupata fedha nyingi zaidi. Katika msimu hii kumefanyiwa marekebisho mapungufu yote yaliyojitokeza katika mkataba uliopita na hata kwenye baadhi ya mechi mliona kulikuwa na changamoto mbalimbali na tupo kwenye hatua za.mwisho kuzirekebisha.

"Kumekuwa na changamoto nyingi sana zilizojotokeza kipindi cha mkataba wetu wa awali lakini tumezifanyia kazi na kwa sasa zipo kwenye hatua za mwisho za kuzimalizia ikiwemo vifaa na hata majukwaa ambayo yatakayokuwa yanatumika kwa ajili ya kuwekea camera kwani viwanja vingi sio rafiki kwa kazi yetu, "amesema Mhando.

Kwa upande wa TFF, Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema kuwa hii ni hatua nzuri kwao pia na hata kwa vilabu kwani mkataba umeboreshwa na sasa hivi watafaidika sana. Mkataba huu wa miaka mitano kwa mwaka kila timu itachukua zaidi ya milioni 120.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...