MAMLAKA ya Mapato Tanzania(TRA) itaendelea kudhibiti na kupambana na  wanaofanyabiashara za magendo katika vituo mbalimbali ambavyo vinaendelea na vitendo vya magendo.

Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema TRA imefuka lengo la Makusanyo ya kodi kwa mwaka 2015/2016. 

Amesema TRA itazidi kupambana na kuziba mianya yote ya  upotevu wa mapato hususani katika msisitizo wa matumizi wa Mashine za Kieletroniki za kodi za EFDs pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara na kufuatilia madeni.

Pia amesema kuwa TRA itaendelea kudhibiti wafanyabiashara wanaokwepa kutumia mashine za Kieletroniki za kodi za (EFDs) kwa kuwakamata na kuwatoza faini au kuwafikisha mahakamani na kuwachukulia hatua za kisheria ili kuhakikisha inafikia na kuvuka malengo.

Amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imeshagawa mashine za Kieletroniki za EFDs 1120 kwa wafanyabiashara wanaostahili kupata mashine hizo bure na ambao hawajachukua machine za kieletroniki za kodi za EFDs ili kuwezesha TRA kukusanya mapato ya Serikali.


 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata(Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuvuka lengo la makusanyo ya Kosi kwa mwaka 2015/2016.Kulia ni Kamishna wa mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Elijah Mwandumbya.
Kamishna wa mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Elijah Mwandumbya akifafanua juu ya Operesheni ambayo itatumika katika makusanyo ya ndani ambapo watapita nyumba kwa nyumba na mtaa kwa mtaa na fremu kwa fremu katika kugawa Mashine za Kieletroniki za EFDs kwaajili ya Kukusanya kodi kwa kila Mfanyabiashara Kushoto ni  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata.
Kushoto ni Kamishna wa mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Elijah Mwandumbya na Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo wakiwa katika mkutano wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...