Zoezi la uhakiki wa vyama vya Siasa visiwani Zanzibar litaanza  Julai 11 mwaka huu baada ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kukamilisha zoezi la kuhakiki vyama vya siasa 21 kwa upande wa Tanzania Bara .
Uhakiki wa Vyama utafanyika katika Ofisi za Vyama zilizopo Zanzibar kwa maana ya Unguja na Pemba.
Zoezi hilo litajumuisha uhakiki wa idadi ya wanachama ambao Chama cha Siasa kinapaswa kuwa nao kwa mujibu wa masharti yalipo kwenye Sheria ya Vyama vya Siasa yam waka 1992.
Zoezi hili ni moja kati ya shughuli za kawaida za Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambalo hufanyika maramoja kila mwaka likilenga kufahamu utekelezaji wa masharti na matakwa ya sheria ya vyama vya siasa.
 Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Bi. Monica Mwailolo (kushoto) akikagua taarifa za Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) wakati wa zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Magomeni Jijini Dar es salaam, katikati ni Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Bi. Nancy Mrikalia akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Augustine Mrema.
 Bi. Esther Mwanri, Mwanansheria kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHAdema) mara baada ya zoezi la uhakiki  katika ofisi iliyopo Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Bw. Willy Brown Nyantiga, Mhasibu kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini akielezea jambo wakati wa zoezi la uhakiki ulioanyika katika Ofisi za Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD). Kulia ni Mwenyekiti  Taifa wa chama hicho Bw.Kamana Masoud na  Kushoto ni Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa” Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa Umma”” Bibi. Piencia Kiure 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...