Wajasiriamali wakubwa kwa wadogo wametakiwa kujitokeza kwa wingi kutumia fursa zilizopo ili waweze kuwezeshwa mitaji ili wawekeze katika shughuli za maendeleo ili kupunguza tatizo la ajira hapa nchini na kusaidia juhudi za serikali na wadau kuleta maendeleo hapa nchini.

Hayo yalisemwa na Balozi wa Japan hapa nchini Bwana Masaharu Yoshida alipokua akifungua semina ya wadau wa maendeleo iliyojadili uwezeshaji wa mitaji kwa wajasiriamali kwa ajili ya shughuli za maendeleo iliyofanyika jana (5/6/2016) jijini Dar es Salaam. 

Semina hiyo iliyoandaliwa na shirika la ushirikiano na maendeleo la Japan (JICA) pamoja na taasisi ya sekta binafsi hapa nchini (TPSF) ilihudhuriwa na mashirika na taasisi za kifedha pamoja na wajasiriamali kutoka sekta binafsi. 
Mkurugenzi wa kitengo cha Africa wa JICA, Hideki Watanabe akielezea Jinsi JICA wanavyofanya shughuli za Maendeleo Afrika

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, watoa mada walionesha kuwa kuna fursa kubwa kwa watanzania wote walioamua kuwa wajasiriamali kwa kufungua viwanda vidogo kwa vikubwa, wakulima na wafanyabiashara kutumia mashirika na taasisi za fedha kujipatia mikopo nafuu ili kuwezesha kukuza biashara na viwanda vyao na wanaweza kulipa kwa muda mrefu kwa riba nafuu. 

Semina hiyo ilibainisha kuwa changamoto kubwa ni kutokua na taarifa kwa watanzania wengi na hivyo kuogopa kuwekeza kwa kutumia taasisi za fedha jambo lililoungwa mkono na washiriki wengi kwani imebainika kuwa ni asilimia 16 tu ya watanzania wanatumia huduma za kibenki hivyo wameaswa kubadilika waweze kunufaika na mitaji ambayo ipo lakini hakuna wanaokidhi vigezo ambapo wanaofuatilia na kunufaika ni watu wachache. 
Mdau kutoka Namaingo Bi. Mariam akichangia jambo

Mwavuli wa wajasiriamali wa Namaingo (Namaingo Business Agency) ni moja ya taasisi zilizohudhuria na ziliahidiwa kupewa ushirikiano na wadau wote wa kuwasaidia kufikia malengo yao kwani mitaji ipo na Namaingo inakidhi vigezo vyote vya kukopesheka kwani mpango kazi wake uko kitaalamu na ushiriki wa serikali na taasisi zake unaifanya iwe mkombozi kwa watanzania wengi maskini. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...