Gari ya Mzunguko a.k.a Daladala limegongana uso kwa uso na Bajaji eneo la Mwaji Uyole Jijini Mbeya kutokana na kile ambacho mashuhuda wameelezea kuwa ni ubabe wa madereva wote kuzidiwa kutokana na mwanga mkali wa taa waliowashiana na kupelekea kupoteza muelekeo kisha kugongana usiku huu...

Bajaji iliyogongana na Gari ya Mzunguko al maarufu kwa Jina la Daladala linalotoka Stendi kuu ya Soko Matola kuelekea Uyole Igawilo ikiwa nyang'anyang'a baada ya kugongana uso kwa uso eneo la Mwaji Uyole Jijini Mbeya usiku huu.



Tunajiuliza vyanzo vya ajali kila siku. Hili nilisemee na wanaohusika kusimamia walishughulikie. Tuka katikati ya mji na mtu anawasha taa za gari lake FULL LIGHT. Hii nayo ni chanzo kimojawapo cha ajali barabarani. Mtu anaendesha gari katikati ya mji amewasha mpaka SCOUT LIGHTS za gari lake! Hili nalowahusika walichukue na kulifanyia kazi. Kwani enyi wahusika wa usimamizi wa njia kwani si inajulikana kiwango gani cha taa zinatakiwa mjini na nje ya mji? Kwani si kun viwango? Au hata hili nalo mpaka Rais alitolee hotuba. Hebe jamani tuwe wabunifu na tuzipende kazi zetu. Wenye walipowewa dhamana ya kusgughulikia haya hebu jaribuni kutazaman hili. Tumezoea kuwaona ao wasimamaizi wa barabarani tu mpaka asaa 12 jioni. Baada yahapo etiserikali inaenda kulala. Tunaiomba serikali yetu, kwa heshima na taadhima hao wasimamizi waliopewa dhamana hiyo wafanye kazi masaa 24 na kuyaona haya tunayoyazungumzia kuhusu uwashaji wa taa na utumiaji wa barabara saa za usiku.
ReplyDelete