Ankal akiwa na keki yake aliyozawadiwa na familia yake katika kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa leo. Anamshukuru Mola kwa kumwezesha kufikisha siku hii adhimu na anaendelea kumuomba amjalie afya njema na baraka tele. Pia anaishukuru familia yake, ndugu, jamaa, marafiki, majirani na wafanyakazi wenzake pamoja na makamanda wa tasnia ya habari kwa salamu za heri walizomtumia.
Wote anawaambia amezipokea salamu hizo kwa kuguswa moyoni na kuwaahidi kuendelea kuwa "mtoto mzuri" na kuendeleza libeneke la Globu ya Jamii ambayo mwezi Ujao Septemba 8 itatimiza miaka 11.
Keki imetengenezwa SWEET HANDS DELIGHT ya Kawe karibu na Kanisa Katoliki. Namba zao 0713 925071/0714 590165
Keki imetengenezwa SWEET HANDS DELIGHT ya Kawe karibu na Kanisa Katoliki. Namba zao 0713 925071/0714 590165
KEKI HAITENGENEZWI, BALI HUWA INAOKWA! KEKI IMEOKWA.......
ReplyDeleteDr Bitozi.
Ankali tunakutakia kila la heri,afya bora na maisha marefu, ombi letu tunaomba FULANAZZZZ ya blogu ya jamii irudi uliongoni
ReplyDeletewadau FFU-ughaibuni
KILA LA HERI,LAKINI MIAKA MINGAPI VILE??
ReplyDeleteMiaka mingapi Ankal au ni siri? Hongera
ReplyDeleteHii kamera hapo juu nayo ni ubunifu wa mpiga keki au imepambwa tu.
ReplyDeleteHappy Birthday Ankal
ReplyDeleteAmefikisha miaka mingled?
ReplyDeleteAnkal ana miaka 47 sasa.
ReplyDelete