Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN ameitaka Taasisi ya Hans Seidel Foundation isaidie kupeleka elimu ya uraia bungeni ili wabunge wajue wajibu wao ndani na nje ya Bunge.

Mheshimiwa SAMIA ametoa kauli hiyo leo baada ya kukutana na ujumbe wa Taasisi ya Hans Seidel Foundation uliomtembelea ofisi kwake Ikulu, Jijini Dar es salaam kutaka kujua kama ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna sheria na kanuni za kuendesha vikao vya Bunge.

Makamu wa Rais aliueleza ujumbe huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa Hans Seidel Foundation Prof. URSULA MANNK kuwa sheria na kanuni zipo za kuendesha vikao vya Bunge lakini baadhi ya wabunge hawazifuati kama inavyotakiwa. Alisema kwa mtazamo wake elimu ya uraia itasaidia katika kuwafanya wabunge hao wajenge nidhamu katika michango na ushiriki wao kwa ujumla ndani na nje ya Bunge.

Akizungumzia kuhusu kuanzishwa kwa dawati la jinsia katika vituo vya polisi Mheshimiwa Samia alisema ni hatua nzuri kwani wanawake kwa sasa wako huru kueleza wanapofanyiwa ukatili wa kijinsia tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

"Kwa sasa wanawake wanakutana na wanawake wenzao wako huru kuzungumza wanaporipoti matukio ya kupigwa na haki inatendeka bila ya hata kutoa rushwa. Kuna mabadiliko ndani ya Jeshi la Polisi kwa upande huo," alisema SAMIA

Alisema kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha watu wote wanaoenda kinyume na taratibu wanachukuliwa hatua za kisheria na kusema kwenye utumishi wa umma mambo yamebadilika kiasi kwamba makusanyo ya kodi yameongezeka serikalini.

Taasisi ya Hans Seidel Foundation yenye makao yake makuu Munich, nchini Ujerumani ambayo inajishughulisha na masuala ya demokrasia, amani na maendeleo huku ikitoa kipaumbele kwenye elimu ya uraia inaendesha shughuli zake katika nchi zaidi ya 60 duniani.

Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam11/08/2016

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...