Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amepiga marufuku matumizi ya mafuta ya transfoma kwa ajili ya kukaangia chips na kutengeneza mikorogo.
Profesa Muhongo ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wakazi wa kijiji cha Kirongo wilayani Muheza mkoani Tanga alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika mkoa huo.
Hii inatisha kweli, tuko salama na mafuta haya?
ReplyDeleteNdani ya Ziwa Victoria Ktk visiwa vya wavuvi, nywele za binadamu hutu mika kukaushia samaki!
ReplyDeleteKwani kabla ya kupigwa marufuku yalikuwa yanaruhusiwa kutumika? Nilidhani polisi badala ya kuwafuatilia original comedy na minguo inayofanana nao wangewakama hao watumiaji wa mafuta ya transforma ambayo yanaua watanzania wengi kila siku. Lakini wenzetu polisi wanaipa kipaumbele vitu vidogo vidogo.
ReplyDeletendio maana kasi ya kansa imezidi Tanzania. Tunatumiaje mafuta ya transfoma wakati mafuta ya alizeti hayana cholesterol na yanapatikana kwa bei nafuu??
ReplyDelete