Mshindi
wa Promosheni ya Bia ya Asili ya Nzagamba inayowawezesha wanywaji wa
Bia hiyo kujishindia Ng'ombe kila wiki kwa mkoa wa Mwanza, Juma John
(kushoto) mkazi wa Kisesa Mkoani humo akipokea zawadi yake ya Ng'ombe
Dume la Nzagamba kutoka kwa Mkuu Kiwanda cha Nzagamba Jijini Mwanza,
Herbat Kilembo (kulia) mara baada ya kuibuka Mshindi kwa wiki ya kwanza
ya Promoseni hiyo. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa Bia ya Asili ya
Nzagamba, Oscar Shelukindo (mwenye Miwani) pamoja na Meneja Mauzo wa Bia
ya Asili ya Nzagamba, Fred Kazindogo.
Mshindi wa Promosheni ya Bia ya Asili ya Nzagamba inayowawezesha
wanywaji wa Bia hiyo kujishindia Ng'ombe kila wiki kwa mkoa wa Mwanza,
Juma John akikabidhiwa zawadi yake ya Ng'ombe mbele ya halaiki wa wakazi wa jiji la Mwanza.
Watumiaji
wa kinywaji cha Nzagamba mkoani Mwanza kwenye eneo la Igoma
wakifuatilia shindano la kumtafuta mshindi wa Dume la Ng'ombe "Nzagamba"
linaloendeshwa na kinywaji cha Nzagamba kwenye mikoa ya kanda ya ziwa.
Nimepata wazo. Tuanzishe mashindano ya kusoma vitabu vya kuelimisha, kwa kila wilaya, na washindi wapate angalau mbuzi au jogoo. Ninajitolea kuchangia mbuzi watano na majogoo kumi kila mwaka.
ReplyDelete