 |
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru uliopokelewa katika Jiji la Arusha eneo la Kisongo kwa ajili ya kukimbizwa kwa siku moja katika urefu wa Kilometa 81.19 katika Tarafa tatu. |
 |
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Athumani Kihamia akipokea Mwenge wa Uhuru ambao utakimbizwa ukiwa unaelimisha na kueneza ujumbe wa "Washirikishwe na Kuwezeshwa" ujumbe huo ukiwa umeambatana na kauli mbiu "Vijana ni Nguvukazi ya Taifa Washirikishwe na Kuwezeshwa" |
 |
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa,George Mbijima akizindua Kituo cha Afya katika Kata ya Elerai jijini Arusha kitakachowahudumia wananchi wa Kata hiyo,Sombetini na Ngarenaro. Miradi yenye thamani ya zaidi ya Sh 1.5 ambayo Soko,Afya,Maji,Elimu,Uwezeshaji wa wananchi kiuchumi makundi maalumu,Ujenzi wa daraja na usafi na utunzaji wa mazingira. |
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Dagarro akikabidhi mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe Iddi Hassan Kimanta baada ya mwenge huo kumaliza kwa mafanikio mbio zake wilaya ya Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...