MFUKO wa Pensehni wa PSPF, umeendelea kusajili wanachama wapya kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSS, wakati wa Maonyesho ya taasisi na makampuni ya kutoa huduma yaliyoandaliwa na Kampuni ya simu za mikononi, Airtel na kwenda na jina la Airtel Bazzar na kufanyika makao makuu ya kampuni hiyo Morocco jijini Dar es Salaam, Agosti 12, 2016.

Akizungumza na waandishi wanhabari kwenye banda la Mfuko huo, Mkuu wa Kitengo cha Usajili nwa Wanachama cha Mfuko huo, Bw. Msafiri S. Mugaka, alsiema, PSPF kupitia mpango wake wa PSS, imefanikiwa kusajili wanachama wapya kadhaa, ambayo ilikuwa ni moja ya huduma walizokuwa wakizitoa kwenye maonyesho hayo ya siku moja.

"Pia wanachama wetu waliweza kuja na kupatiwa huduma za taarifa za michango yao, wanawezaji kufaidika na mafao mbalimbali ya yatolewayo na Mfuko kama vile fao la Elimu, Uzazi, mikopo kwa wafanyakazi wapya, na mafao mengine kadhaa,"alisema.

Maonyesho hayo yalishirikisha makampuni kadhaa ya kibinafsi na taasisi za umma na yalilenga kuwakutanisha wateja wa Airtel, na taasisi hizo ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wenyewe wa Airtel kutembelea taasisi hizo na kupatiwa huduma mbalimbali wakiwa hapo hapo kazini. 

Mkuu wa kitengo cha kuandikisha wanachama cha Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Msafiri S. Mugaka, akiwapatia maelezo wanachama hawa wa PSPF, kuhusu mafao na faida nyingi ambazo mwanachama anaweza kupata ikiwa ni sehemu ya huduma zitolewazo na Mfuko.

Elimu ikiendelea kutolewa kuhusu huduma za Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kwa wananchi waliotembelea banda la Mfuko huo

Penzila Kaisi (kulia), Afisa Matekelezo msaidizi wa PSPF, akimuelimisha mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo ili kujua shughuli zake.

Angelina akitoa somo kwa mwananchi huyu.

Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Maseka Kadala, (kulia), akimsikilzia kwa makini mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo ambapo baadaye alijiunga baada ya kuelewa huduma za Mfuko huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...