Wanamuziki
wa Bendi ya Sikinde Ngoma ya Ukae, wakiyarudi magoma katika Tamasha la
wazi la Muziki lililofanyika kwenye Viwanja vya NAFASI, Mikocheni jijini
Dar es salaam Agosti 27, 2016. Tamasha hilo ni muendelezo wa matamasha
ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi katika eneo hilo, huku hilo likiwa
na upekee, kwani lilihusisha uzinduzi wa Nyimbo mpya mbali mbali za
Bendi tatu tofauti ambazo ni Sikinde wenyewe, Cocodo pamoja na The
Spirits kutoka Bagamoyo Mkoani Pwani. Ilikuwa ni burudani ya aina yake
yenye kuvutia wengi waliofika kwenye eneo hilo maarufu kwa kazi mbali
mbali za Sanaa.
Wanamuziki wa Bendi ya The Spirits kutoka Bagamoyo Mkoani Pwani wakifanya yao jukwaani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...