Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akikagua kuku waliofungwa kisasa ambapo jogoo mmoja aliyefikisha umri wa mwaka mmoja anauzwa shilingi 20,000.

Na Mathias Canal

Wananchi wametakiwa kujihusisha na ufugaji wa kuku kwa njia za kisasa ili waweze kujipatia kipato kupitia mayai ama kuuza kuku mwenyewe ili kuondokana na dhana ya kuishi na kuku ilihali wanajigamba kama wafugaji wazuri.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida Miraji Jumanne Mtaturu alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi katika maonesho ya Nane nane yanayofanyika katika Uwanja wa Nzuguni Kanda ya Kati Dodoma ambayo yanataraji kufikia kilele hapo kesho.

Mtaturu amesema kuwa asilimia kubwa ya wananchi Wilayani humo na Taifa kwa ujumla wanajihusisha na shughuli za Kilimo na ufugaji lakini aina ya ufugaji wanayoitumia ni ile iliyopitwa na wakati ya kuishi na mifugo ndani badala ya kuijengea eneo la banda ambalo ni pana na maalumu kwa ajili ya ufugaji.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akipata maelekezo ya ufugaji wa kisasa wa kuku  kutoka kwa mfugaji aliyefanikiwa katika ufugaji Madai Njou anayetokea Kijiji cha Nyangwe, Kata ya Iseke baada ya kupatiwa mafunzo kutoka Idara ya Kilimo na ufugaji ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.

Dc Mtaturu amewataka wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi katika idara ya kilimo kutoa elimu kwa wananchi juu ya mazao makuu ya biashara yanayostahimili mvua ili kupata mazao ya kutosha na kuyauza kwa wakati tofauti na mazao mengine ambayo yanalimwa kila maeneo hivyo kupunguza gharama halisi ya bei.

Amewataka pia wataalamu hao kuhakikisha elimu wanayoitoa kwa wananchi inakuwa sambamba na kuwashauri wananchi kulima zao la mtama wa muda mfupi aina ya Hakina na Macia.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akikagua Tomato Saurce inayotengenezwa na mjasiriamali Rehema F. Maliwa na nyanya aina ya Tanya.

Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ayoub Yusuph amesema kuwa ofisi yake itatekeleza maagizo yote yaliyotolewa na mkuu wa Wilaya hiyo ili kuwainua zaidi wananchi ambao wanalima na kufuga lakini sio kilimo na ufugaji wa kisasa jambo ambalo linawarudisha nyuma kimaendeleo.

Yusuph alisema kuwa katika maonesho hayo wamewaalika wakulima na wafugaji ambao wamefanikiwa katika kilimo na ufugaji wao baada ya kupata mafunzo kutoka katika ofisi yake ili kushuhudia na kuelezea mbinu walizopatiwa na namna zilivyowasaidia.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...