Na Mwandishi Wetu
Wazazi
nchini wametakiwa kuwa na moyo wa kujali afya za watoto wao hasa
zinapotokea fursa za tiba za bure kwenye jamii zao kwani ni nadra sana
kwa fursa hizi kujitokeza katika jamii za kitanzania.
Hayo
yamesemwa na mbunge wa Chalinze Mhehimiwa Ridhwani Kikwete
alipotembelea kambi ya madaktari Bingwa wa Mifupa na mishipa ya fahamu
kutoka taasisi ya MOI ambao wako katika kambi tiba ya GSM Foundation,
inayozunguka nchi nzima kuwafanyia upasuaji watoto waliozaliwana vichwa
vikubwa na mgongo wazi.
Mbunge
wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akipata maelezo kutoka kwa
Mtaalamu wa nusu Kaputi, Bw. Ogutu Ogonga mara baada ya kutembelea kambi
ya madaktari Bingwa wa Mifupa na mishipa ya fahamu kutoka taasisi ya
MOI ambao wako katika kambi tiba ya GSM Foundation, inayozunguka nchi
nzima kuwafanyia upasuaji watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa na
mgongo wazi mapema leo Mjini Kibaha - Pwani.
Huu
ni mkoa wa 10 kwa kambi hii kutembelea, huku ukiwa ni msimu wa tatu wa
kambi tiba hizi zenye lento la kuokoa miasma ya watoto takriban 3500
wanaohisiwa kupoteza maisha kila mwaka köa mujibu wa tafiti za MOI za
mwaka 2002, ambazo zinasema zaidi ya watoto 4000 huzaliwa kila mwaka
lakeni ni 500 tu huweza kufika kwenye tiba huku changamoto kubwa
ikitajwa kuwa ni uchache wa madaktarim ba ukubwa wa gharama za tiba.
Awamu
ya kwanza ya kambi tiba ya GSM ilipita mikoa ya Mwanza, Shinyanga.
Singida, Dodoma na Morogoro. Ya pili ikapita Mtwara, Songea, Mbeya na
iringa. Hii awamu ya tatu itapita katika mikoa ya Pwani, Tanga,
Kilimanjaro na Mara.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiongea na
Kaimu Mganga Mkuu hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani - Tumbi, Dk Aggey
Geoffey(Wa pili kutoka kushoto), na Dk Silas Msangi(
Wa kwanza kushoto), mara baada ya kutembelea kambi ya madaktari Bingwa
wa Mifupa na mishipa ya fahamu kutoka taasisi ya MOI ambao wako katika
kambi tiba ya GSM Foundation, inayozunguka nchi nzima kuwafanyia
upasuaji watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi mapema leo
Mjini Kibaha. Kulia ni Afisa uhusiano wa GSM Foundation Khalphan
Kiwamba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...