Mkurugenzi
wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji akifafanua zaidi kuhusu kampeni ya
USIKATE TAMAA,jijini Dar leo .
Mwanamuziki, Nurdin Bilal Ali maarufu kama Shetta akielezea safari yake ya muziki hadi kufika hatua aliyopo sasa, ambayo binafsi amekiri kuwa kwake ni mafanikio makubwa. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL
Group, Fatema Dewji akizungumza kuhusu kampeni ya USIKATE TAMAA, Kushoto
ni mwanamuziki Shetta na kulia na Kaimu Meneja Masoko wa Mohammed
Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Zainul Mzige.PICHA NA MICHUZI JR.
kampuni ya Mohammed Enterprises
Tanzania Limited (MeTL Group) leo imefanya uzinduzi wa kampeni ambayo
imepewa jina la USIKATE TAMAA ikiwa na lengo la kuhamasisha watu
waliokata tamaa kuwa nao wana nafasi ya kufanikiwa.
Akizungumzia
kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji alisema
kuwa kampeni hiyo inalenga kuleta matumaini mapya katika jamii kwa watu
ambao wamekuwa wakipoteza matumaini kutokana na hali ya ugumu wa
kimaisha ambayo imekuwa ikiwakabili.
Alisema
kampeni hiyo itakuwa ikitumia watu mbalimbali ambao wamefanikiwa na
watakuwa wakitoa historia zao katika maeneo mbalimbali ambayo
watatembelea, wakielezea jinsi walivyokuwa na maisha magumu hapo awali
na sasa wamefanikiwa kimaisha.
“Kuna
watu hawana uwezo na wanazungukwa na watu ambao wamekuwa wakiwaambia
kuwa hawawezi kufanikiwa lakini kupitia kampeni ya USIKATE TAMAA
wataweza kupata matumaini kutoka kwa watu ambao walipita katika maisha
magumu na baadae wakafanya vyema,” alisema Fatema.
Mkurugenzi
wa masoko huyo aliongeza kuwa kampuni ya MeTL pamoja na kufanya
biashara lakini pia inaijali jamii na inapenda kuona watu wakifanikiwa
kimaisha hivyo kupitia kampeni ya USIKATE TAMAA itaweza kusaidia watu wa
aina mbalimbali waliopo katika jamii ya kitanzania wakipata matumaini
mapya na kuongeza juhudi ili wafanikiwe.
“MeTL
kupitia chapa yake ya MO inataka kuona watu wakiendelea kupambana na
kufanikiwa, tunataka watu wafanikiwe na tuwape tuzo, tuwape sauti ya
kusikika na huu ni mwanzo tu, kampeni hii itafanyika kwa muda mrefu
zaidi,” alisema Fatema.
Kwa
upande wa mwanamuziki, Nurdin Bilal Ali (Shetta) ambaye ametumika kama
mmoja wa watu ambao wamefanikiwa, alielezea safari yake ya kimuziki na
kusema kuwa awali alikuwa akiishi kwa moja ya wasanii wa muziki nchini
na alikuwa akifanya kazi za nyumbani kwa mtu huyo lakini akiwa na nia ya
kutafuta njia ya kutoka kimuziki na juhudi alizozionyesha zimemwezesha
kuwa moja ya wasanii waliofanikiwa nchini.
“Unaweza
kuwa unajiamini katika kipaji chako lakini bado watu wanakudharau, mimi
nimewahi kuishi na mwanamuziki mkubwa nchini lakini najijua nina kipaji
lakini kwakuwa nilikuwa natafuta njia ya kutoka kimuziki ilinibidi
nifanye hivyo,“Ilikuwa
naosha gari lake, naosha vyombo na hata kumwogesha mdogo wake lakini
nilikuwa najua nini nafanya na nini nataka, msanii yule alikuwa
anafahamiana na watu wengi na mimi ikanisaidia kupata njia ya kutokea na
leo kwa hatua niliyofikia nimefanikiwa,” alisema Shetta.
Hivi huwa ni mwiko kwa wanamziki wa bongo flava kukata nywele au kuchana nywela kawaida!
ReplyDelete