Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akipokea msaada wa fedha cha dola laki mbili za Kimarekani (USD 200,000) -takriban Tshs. 437,000,000/- taslimu kutoka kwa
Balozi wa Uganda hapa nchini Mhe. Doroth Samali Hyuha ( wa pili kutoka kushoto) akiwa
pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Elibariki Maleko. Msaada huo
umetolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kuwasaidia
waathirika wa Tetemeko la ardhi mkoani Kagera leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi mchango wa fedha cha dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) - takriban Tshs. 437,000,000/- taslimu uliotolewa na Rais wa
Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kusaidia waathirika watetemeko la ardhi mkoani Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akimshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kusoma
taarifa kuhusu Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Naibu
Balozi wa Kenya hapa nchini Mhe. Boniface Muhia mara baada ya kupokea salamu za pole
kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na kwa misaada mbalimbali ya mabati 4,000 na vifaa vya majumbani ikiwemo magodoro na mashuka ambayo
inatarajiwa kuwasili mkoani Kagera kutoka Kenya muda wowote kuanzia sasa. Katikati ni Balozi wa Uganda hapa nchini Mhe. Doroth Samali Hyuha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara
baada ya kupokea msaada wa fedha dola laki mbili za Kimarekani (takriban Tshs. 437,000,000/- ) taslimu kutoka Uganda pamoja na taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera kutoka
kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
Asanteni sana kwa wema wenu majirani zetu. Mmetoa kwa moyo pamoja na kujuwa kuwa raia wenu wana mahitaji pia. Mungu awaongezee na awape amani itokayo Kwake.
ReplyDelete