.Mkurugenzi wa Uhamasishaji Sera na Utafiti wa TPSF,Gili Teri
akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wakujadili Agenda maalum
inayohusisha masuala mbalimbali yakiwemo ya Kilimo,Nishati,Elimu na
mengineyo.
.Baadhi ya Wadau wa Sekta Binafsi na Wafanyabiashara wakiwa katika semina hiyo.
Taasisi ya Sekta Binafsi nchini(TPSF) imekutana na
Wafanyabiashara pamoja na wadau wa Sekta Binafsi ili kutengeneza Agenda
ya Biashara ya Taifa.
Agenda hiyo ina lengo la kukusanya maoni pamoja na
matarajio ya wadau wa Sekta Binafsi hususan kuelekea katika Uchumi wa
Viwanda miaka 5 na 10 ijayo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika semina maalum
iliyowakutanisha Wadau wa Sekta Binafsi,Mkurugenzi wa Uhamasishaji Sera
na Utafiti wa TPSF,Gili Teri amesema Agenda hiyo inahusisha masuala
mtambuka lakini masuala halisi ya Kisekta yakiwemo ya
Kilimo,Nishati,Elimu na Sekta nyingine mbalimbali.
"Mazingira ya Biashara yanapoboreshwa mimi na wewe
tunaofanya biashara tunaweza kufaidika zaidi,tukaajiri watu wengi na
tukalipa kodi zaidi,"amesema Teri
Amesema wanatengeneza agenda ya pamoja ambayo itatumika
kama kitu cha ambacho kitaongoza mawasiliano kati ya Sekta Binafsi
pamoja na wadau wengine wakiwemo Serikali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...