Na Bodi ya Filamu
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nnape Nnauye amesisitiza kuwa
wasambazaji wote wa filamu kutoka nje lazima waingie mikataba na wazalishaji wa
filamu watakazotaka kuzisambaza nchini. Kauli hiyo ya Waziri Nnape ameitoa
kwenye kikao baina ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na jumuiya
ya wasambazaji wa filamu kutoka nje kilichofanyika leo jijini Dar es salaam.
Waziri
Nnape amesema “kuingia mikataba na wazalishaji wa filamu ni takwa la kisheria
lisiloepukika”. Aliendelea kusisitiza kwamba kazi ya serikali ni kuhakikisha
inasimamia sheria hata kama sheria hizo zitakuwa haziwafurahishi walio wengi.
Kikao
hicho baina ya Waziri Nnape na wasambazaji wa filamu kutoka nje ni mwendelezo
wa vikao vya kurasimisha tasnia ya filamu nchini. Awali Waziri Nnape aliwaagiza
watendaji wa wizara yake pamoja na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kwa
pamoja na jumuiya ya wasambazaji wa filamu kutoka nje kuunda kamati ndogo ambayo
itakuwa na kazi ya kujadili changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili
wasambazaji wa filamu za nje na kuzitolea ufumbuzi.
Ikumbukwe
mwezi Julai Waziri Nnape pamoja na Bodi ya Filamu Tanzania walifanya operesheni
ya kukamata kazi bandia za wasanii. Kwenye zoezi hilo mitambo ya kudurufu kazi
za wasanii na zaidi ya santuri(CD na DVD) 600,000 zilikamatwa. Baada ya zoezi
hilo wasambazaji wa filamu kutoka nje kupitia jumuiya yao na mbunge wa Ilala Mussa
Azzan waliomba kukutana na uongozi Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo. Baada ya kikao kufanyika Waziri Nnape aliagiza iundwe kamati ndogo
itakayoshughulikia changamoto zinazowakabili wasambazaji wa filamu za nje chini
ya uenyekiti wa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania.
Kwa
upande wake Mbunge wa Ilala Mussa Azzan (zungu) amewataka wasambazaji hao
kuheshimu maazimio waliyoyafikia baina yao na serikali kupitia kamati ndogo
iliyoundwa na Mheshimiwa Nnape.
WAZIRI
WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE
AKISISITIZA JAMBO KWENYE KIKAO NA WASAMBAZAJI WA FILAMU ZA NJE. MHESHIMIWA
NNAPE AMEWAASA WASAMBAZAJI WA FILAMU ZA NJE KUHAKIKISHA WANAINGIA MIKATABA NA
WAZALISHAJI WA FILAMU WANAZOTAKA KUZISAMBAZA HAPA NCHINI KWANI NI TAKWA LA
KISHERIA LISILOEPUKIKA.
1. MBUNGE
WA ILALA MHESHIMIWA MUSSA AZZAN (ZUNGU) AKIZUNGUMZA NA WASAMBAZAJI WA FILAMU
KUTOKA NJE(HAWAPO PICHANI) AMBAO WALIHUDHURIA KIKAO BAINA YA JUMUIYA YA
WASAMBAZAJI WA FILAMU ZA NJE NA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO.
KWENYE NASAHA ZAKE MHESHIMIWA ZUNGU ALIWAASA WASAMBAZAJI WA FILAMU ZA NJE
KUTEKELEZA MAAZIMIO YALIYOFIKIWA.
1. BAADHI
YA WASAMBAZAJI WA FILAMU KUTOKA NJE WAKIMSIKILIZA WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI,
SANAA NA MICHEZO NNAPE NNAUYE WAKATI WA KIKAO CHA KUTATUA CHANGAMOTO
ZINAZOWAKABILI WASAMBAZAJI HAO.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...