MKURUGENZI
Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda
Sanga akizungumza kabla ya ufunguzi wa mafunzo hayo alisema TAMWA ina
kila sababu ya kuingia katika mapambano ya ajali nchini kwa kuwa
zimekuwa zikiwaathiri wanawake na watoto kwa kiasi kikubwa.
Alisema
licha ya ajali nyingi kupoteza maisha ya wanaume na kujeruhi wengine
kundi hilo limekuwa likiwaacha wake zao na watoto pasipo na msaada kwa
kuwa wengi humtegemea baba kama mtafutaji katika familia.
Alisema wanawake wanaoachwa peke yao na familia wamekuwa wakibeba mzigo
mkubwa wa familia jambo ambalo limeendelea kuwaingiza katika hali ngumu.
Aidha aliongeza kuwa pamoja na hayo ajali nyingi za waendesha pikipiki
maarufu kwa jina la bodaboda zimekuwa zikiwaathiri akina dada na akina
mama ambao ndio watumiaji wa vyombo hivyo vya usafiri kiasi kikubwa.
Tamwa
katika mradi huo imejikita katika kutoa elimu ya madereva kuepuka
ulevi, ufungaji mikanda ya usalama katika magari, mwendo kasi na
matumizi ya kofia ngumu kwa waendesha pikipiki pamoja na abiria wao.
Kwa upande wake Mwasilishaji mada kutoka Safe Speed Foundation, Henry
Bantu alisema suala la usalama barabarani si jukumu la taasisi moja
hivyo kila mtu anapaswa kushiriki katika kupambana na hatimaye
kutokomeza ajali hizo ambazo zimekuwa zikipoteza roho za watu, mali
pamoja na kusababisha ulemavu kwa baadhi ya waathirika wa ajali hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...