Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii asubuhi hii, inaeleza kuwa Bondia maarufu nchini, Thomas Mashali amekutwa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo na mwili wake kukutwa maeneo ya Kimara, Jijini Dar es salaam. akithibitisha kutokea kwa kifo cha mwanamasumbwi huyo, Bondia Abdallah Pazi (Dullah Mbabe) amesema Mashali amefikwa na umauti huo usiku wa kumkia leo kwa kudaiwa kupigwa mpaka kuuawa na watu wasiojulikana kwa tuhuma za wizi. tutaendelea kujuzana taarifa zaidi za msiba huu wa Mwanamasumbwi huyu nguli hapa nchini, endelea kutembelea Libeneke la Globu ya Jamii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...