
Mhe. Nape Nnauye pamoja na watendaji wa Wizara wamepokea kwa
masikitiko makubwa taarifa za kifo cha bondia huyo na kuongeza kuwa kifo hicho
ni pigo katika tasnia ya michezo nchini.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha bondia
Thomas Mashali, sina maneno ya kuelezea masikitiko na huzuni niliyonayo, kwani
kifo chake ni pigo katika tasnia ya masumbwi nchini” alisema Mhe.Nnauye.
Aidha, Waziri Nape Nnauye ameitaka jamii na wanamichezo kote
nchini kuwa wavumilivu na watulivu wakati wote wa msiba na kumuombea marehemu
makao mema kwa Mwenyezi Mungu.
Thomas Mashali alizaliwa Jijini Dar es Salaam tarehe 9 Septemba,
1989 na kuweza kushiriki katika baadhi ya michezo mbalimbali ya masumbwi ya
kulipwa ambapo kati ya michezo 26 aliyowahi kucheza alishinda michezo 19, ambayo
tisa ni ya Knock Out (KO), lakini pia alipoteza michezo mitano yaani KO minne
na kutoka sare mchezo mmoja.
Bondia Thomas Mashali aliwahi kupigana na baadhi ya mabondia maarufu
wa ndani na nje ya nchi wakiwemo Francis Cheka, Abdallah Paziwapazi, Ibrahim
Tamba na wengineo.
Mungu
ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina.
Imetolewa na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo
31 Oktoba, 2016
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...