Beki wa kulia na nahodha wa timu ya Taifa ya Brazil kwenye Kombe la Dunia Mwaka 1970 Carlos
Alberto amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 72, klabu yake ya zamani Santos imetangaza leo.
Beki huyo amechezea Brazil mara 53 na kufunga goli linalotajwa
kuwa bora zaidi katika historia ya Kombe la Dunia kwa kupiga shuti kali
lililomaliozia ushidni wa bao 4-1 dhidi ya Italy kwenye fainali hizo za mwaka
1970 (angalia video hapo juu).
Kwa mujibu wa habari kutoka Brazil Carlos Alberto alifariki kwa
ugonjwa wa moyo. Alipata kuchezea vilabu vya Fluminense, Santos, Flamengo
na New York Cosmos kati ya miaka 1962
hadi 1982 kabla ya kuwa kocha.Taarifa ya klabu ya Santos imesema:
"Carlos amecheza jumla ya mechi 445 na kufunga magoli 40 goals toka
1965-1975, na anasifika kuwa beki wa kulia bora kabisa katika Brazil".
Klabu hiyo imetangaza siku tatu za maombolezo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...