Mradi
mkubwa wa kijiji cha digitali cha Ololosokwan, Loliondo umezinduliwa
rasmi mwishoni mwa wiki, miaka miwili tangu kutiwa saini kwa uanzishwaji
wake kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(Unesco) na kampuni ya Samsung.
Mganga Mkuu wa Wilaya Ngorongoro, Dk. Omari Sukari akitoa maelezo ya huduma mbalimbali za Afya zitakazokuwa zikipatikana ndani ya moja ya makontena ya kijiji cha Kidigitali cha Samsung (Samsung Digital Village) kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo (kulia) wakati wa uzinduzi wa kituo cha huduma maalum za afya uliofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Hiki
kitakuwa ni kijiji cha nne cha digitali barani Afrika cha kwanza kikiwa
nchini Afrika Kusini huku kingine kikiwa Gabon na Ethiopia.Kijiji
hicho cha digitali ni nadharia ya Samsung katika kurejesha faida kwa
umma na kina huduma mbalimbali ambazo zikiunganishwa na haja ya wananchi
zitasaidia kubadili maisha ya wamasai na kuondokana na utegemezi wa
mifugo pekee.
Uzinduzi
rasmi wa kijiji hicho umefanywa na Mkuu wa mkoa Arusha Mrisho Gambo kwa
niaba yaWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto
Ummy Mwalimu.
Kijiji
hicho cha digitali kina shule yenye tehama ikiwa na maunganisho ya
intaneti, kiliniki ya kisasa ikiwa na kituo cha teknolojia ya
mawasiliano yenye kuwezesha utabibu (telemedicine) na jenereta
linalotumia nguvu za jua.
Mradi
huo ambao ulishuhudiwa utiaji saini na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya
Taifa ya UNESCO, Bi. Leah Kihimbi kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo na Dkt. N. Iriya kutoka Shirika la Afya Duniani
(WHO) Dar es Salaam na wafanyakazi wa UNESCO mwaka 2014, kukamilika
kwake kunawezesha UNESCO na serikali ya Tanzania kuwapatia wakazi wa
eneo hilo huduma bora za afya na vijana wa Kimasai nafasi ya kupata
elimu kutokana na ukweli kuwa kwa utamaduni na kazi zao za ufugaji
wamekuwa wakipata shida ya kupata elimu.
Utiaji
saini wake katika mwaka huo ulifanywa na Mkuu wa ofisi na Mwakilishi
Shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Samsung
Electronics nchini Tanzania, Bw. Mike Seo .Kupitia kijiji hicho vijana
wataendelea na masomo hata kama wanachunga mifugo yao kutokana na
kupatiwa tablet ambazo zitawawezesha kujifunza hata wakiwa nje
wakichunga mifugo yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...