Mwanafunzi wa darasa la sita Shule ya Msingi Sombetini Jackson Mutalemwa akiuliza swali baada ya kupata elimu ya Ukatili dhidi ya watoto kutoka Ofisi ya Dawati la Jinsia na watoto mkoani hapa.
Mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Arusha Mkaguzi wa Polisi Happyness Temu akisisitiza jambo kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Sombetini wakati anatoa elimu juu ya Ukatili dhidi ya Watoto kushoto kwake ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Evelyn Simalenga.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Sombetini iliyopo jijini Arusha wakishangilia mara baada ya kupata elimu ya Ukatili dhidi ya Watoto iliyotolewa na kitengo cha Dawati la Jinsia na watoto la mkoani hapa
Askari Polisi kutoka kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Arusha Happy Mshana akiwaelezea wanafunzi wa shule ya Msingi Sombetini iliyopo jijini hapa aina za Ukatili dhidi ya Watoto.
Picha na habari na Rashid
Nchimbi wa Jeshi la Polisi, Arusha
Sina uhakika kama taarifa hii itakufikia wakati muafaka ila kuna matendo yanayo sikitisha yanatendeka eneo la kimandolu juu au kijiji cha sokon two ukweli ni kwamba baadhi ya ushaid upo wazi ila kuna baadhi ha wanandugu wanaingiza undugu wakati unaotendeka hapo ni ukatili wa baba kumuharibu binti yake wakumzaa naomba fuatilia hii mkuu
ReplyDelete