Wilaya ya Tunduru imezindua kampeni ya uchomaji tofali kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa matundu ya vyoo kwenye shule za msingi na sekondari.

Uzinduzi huo umefanywa jana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge alipofanya ziara ya kikazi kijiji cha Ligoma Tarafa ya Namasakata. Katika kuunga mkono juhudi za wananchi mkuu wa Mkoa ameshiriki kazi ya kupanga tanuri la matofali yaliyofyatuliwa na wananchi ili kuwezesha kijiji kujenga matundu ya vyoo kwenye shule ya msingi Ligoma

Katika uzinduzi huu jumla ya matofali 200,000 yamefyatuliwa na wanakijiji cha Ligoma mwezi uliopita ambapo kazi ya uchomaji itatumia Siku kumi na ñne hadi kukamilika. Akitoa taarifa ya utekelezaji a kampeni ya benki tofali kwenye wilaya ya Tunduru mkuu wa wilaya hiyo Juma Homera alisema jumla ya tofali 7,070,000 zimefyatuliwa kwenye Tarafa zote saba za Tunduru
Aliongeza kusema wilaya yake imejipanga kukamilisha zoezi la matofali na kuahidi kuwa ifikiapo mwezi Desemba mwaka huu watakamilisha ujenzi wa vyoo kwani halmashauri kupitia makusanyo ya ndani watatoa vifaa vya kiwandani

Wakati huo huo mkuu wa Mkoa alikagua hali ya matundu ya vyoo kwenye hule ya msingi Ligoma na kujionea upungufu mkubwa wa matundu ya vyoo vya wanafunzi. Shule ya msingi Ligoma yenye wanafunzi 656 na na walimu 8 ina matundu ya vyoo sita na upungufu uliopo ni matundu ya vyoo 24 wakati mahitaji kwa wasichana ni 18 na wavulana ni 12. Dkt. Mahenge amewapongeza wilaya ya Tunduru kwa jitihada walizofikia kupata matofali na kuwataka waanze kuchimba matundu ya vyoo

“Nawataka sasa muanze hatua ya pili kwa kuchimba mashimo ya vyoo ili halmashauri ya wilaya ilete saruji,nondo,mabati,na masinki na kuweka mfumo wa maji” alisisita mkuu wa mkoa.

Mkuu wa Mkoa amewataka na kuwasisitiza wakuu wa wilaya zote kutembelea na kukagua hali ya miundombinu ya vyoo,madarasa na nyumba za walimu ili matofali yanayofyatuliwa sasa na wananchi yatumike kukamilisha ujenzi ya mundombinu hii muhimu. Aidha amewaagiza maafisa Elimu wote wa wilaya kutokaa ofisini na kutayarisha takwimu na zisizo na uhalisia.

Dkt.Mahenge alizindua kampeni ya ufyatuaji tofali kwenye Mkoa wa Ruvuma mwezi Agosti mwaka huu na kuelekeza kijiji vyote kuwa na benki tofali 100,000 zitatumika kujenga matundu ya vyoo kwenye shule,zahanati kwenye kijiji visivyo na zahanati.

Alisema ni lengo la Mkoa kuona unanza mwaka 2017 ukiwa umekamilisha ujenzi na matundu ya vyoo kwenye shule za msingi na sekondari ili kuwawezesha wanafunzi kusoma kwenye mazingira ya usafi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge (aliekuwa chini) akiwa na mbunge wa Tunduru Kusini Idd Mpakate (wa pili kushoto) wakishiriki kazi ya kupanga tanuru la tofali pamoja na wananchi wa kijiji cha Ligoma wilaya ya Tunduru Jana.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt.Binilith Mahenge akikagua kazi ya kupanga tanuru la tofali aliposhiriki uzinduzi wa uchomaji matofali kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo kwa shule ya msingi Ligoma wilaya ya Tunduru Jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...