Meneja Huduma kwa Wateja wa kampuni ya Start My Safari, Joshua Sewe (Kushoto)
akifanunua matumizi ya kifaa maalum kitumikacho katika ukataji wa tiketi za
mabasi katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati
ni Doris Kini Afisa Huduma kwa Wateja na Meneja Maendeleo ya Biashara wa
kampuni hiyo Bw. George Mlambala(Kulia).
Meneja Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya Start My Safari,
Bw. George Mlambala (Katikati) akifanunua matumizi ya kifaa maalum kitumikacho
katika ukataji wa tiketi za mabasi katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Doris Kini Afisa Huduma kwa Wateja na Meneja
Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo Bw. Joshua Sewe (Kushoto).
Kampuni ya Start My Safari Limited imeziwezesha kampuni 25 za
mabasi hapa nchini kuanza kutumia teknolojia mpya ya ukataji wa tiketi kwa
kutumia simu za mkononi na mtandao wa intaneti kuwakatia tiketi wateja wao.
Meneja Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya Start My Safari
iliyoingia makubaliano na wasafirishaji hao, Geoorge Mrambala amesema kuwa, kwa
sasa watanzania wanaweza kukata tiketi
mahali popote na wakati wowote kwa kutumia mifumo hiyo ya mawasiliano.
“Hakuna gharama za ziada katika ukataji wa tiketi, yaani abiria
analipa nauli ileile iliyoidhinishwa na serikali na ndani ya dakika chache
anatumiwa tiketi yake ya kielektroniki,” amesema.
Amesema mfumo huo pia unawafuatilia wateja wao kuanzia
wanapokata tiketi, kabla ya safari, wawapo safarini na wanapoahirisha safari.
Meneja huyo amesema mfumo unamrahisishia msafiri kujua basi
atakalosafiri nalo kama anavyotaka mwenyewe, muda atakaofika na awapo njiani
anafuatiliwa mpaka anapofika aendako.
“Huduma hii kwa sasa inapatikana kirahisi zaidi kwa watumiaji
wa smartphone, lakini pia hata kama hana simu hiyo anaweza kutuma ujumbe mfupi
na moja moja anatumia tiketi na kuunganishwa na basi atakosafiri nalo na
inapatikana pia kwa njia ya mtandao,” alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...