Gharama za upasuaji wa Moyo ni kubwa si chini ya shilingi Millioni 6 za Tanzania. Kwa wagonjwa hawa tunashukuru Wizara ya Afya,Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Medical Centre (BMC) lakini shukurani nyingi ziende MMI ambao wamenunua vifaa vingi ba ambavyo watatuachia hapa, ili tuendelee naupasuaji huu.
Kwa mujibu wa Rais wa Jumuiya ya Shia Imami Islaili Muslims, Kanda ya Magharibi Bw. Altaf Hirani (katikati) amesema kuwa kila mwaka Hospitali ya Aga Khan inatumia shilingi za Kitanzania bilioni 2 kuwahudumia wagonjwa bila malipo yoyote ambapo hadi sasa zaidi ya wagonjwa 600 wamefanyiwa upasuaji wa moyo.
Watanzania madaktari 10 walipelekwa nchi za nje kupata mafunzo zaidi. Aidha Wakfu wa Afya wa Aga Khan umewekeza shilingi za kitanzania bilioni 167 katika ujenzi wa Hospitali ya kisasa ya kutoa mafunzo ya udaktari ambayo tayari imeanza kujengwa.
Pia kujengwa vituo 35 vya afya vitajengwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini, vitano vikiwa katika mkoa wa Mwanza. Kupata zaidi BOFYA HAPA
|
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...