Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles
Mwijage ameipongeza na kuishukuru Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) kwa jitihada za kuendelea kuelimisha
wafanyabiashara kutambua umuhimu wa kulipa kodi
utakaoiwezesha Serikali kusonga mbele katika suala zima na
ukuzaji wa viwanda vya ndani hapa nchini.
Mhe. Mwijage aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano
wa nne wa mwaka wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa
Msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1); uliofanyika tarehe 29
Novemba 2016 katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee jijini
Dar es Salaam.
Mkutano huo uliandaliwa kwa ushirikiano kati ya GS1 na TRA kwa
lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu wadau wao,
kujadili mambo muhimu ya kodi yanayohusu umuhimu wa Namba
ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) katika kuweza kupata
msimbomilia (barcodes 620) na kuweza kuzitambulisha bidhaa za
Tanzania kimataifa pamoja na kuadhimisha miaka mitano tangu
kuanzishwa kwa taasisi hiyo.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage wa tatu kulia akikata keki kuadhimisha mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa Msimbomilia 620 (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini Dar es salaam. Wa kwanza kushoto ni mwakilishi kutoka TRA ambaye ni Afisa Mkuu wa Elimu kwa Mlipakodi Bi. Rose Mahendeka na wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya GS1 Bw. Gideon Mazara wakishuhudia tukio hilo.
Waziri Mwijage aliliagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
kuhakikisha kila mfanyabiashara anayemiliki viwanda vidogo na
vya kati kuhakikisha anakuwa na TIN na namba ya msimbomilia
620 inayotolewa na GS1 Tanzania kabla ya kuhuisha vyeti vyao
vya biashara.
Aidha Waziri Mwijage amesema kuwa uchumi wa viwanda
unatakiwa kukua nchini ili kuweza kuzalisha bidhaa bora
zitakazouzwa ndani na nje ya nchi na kukusanya kodi stahiki
itakayoiwezesha Serikali kutoa huduma bora za kijamii kwa
maendeleo ya wananchi wa Tanzania .
“Ifike wakati wafanyabiashara muwaelewe vizuri TRA na kulipa
kodi stahiki ya Serikali, ili nchi iweze kusonga mbele” alisema
Mhe. Mwijage.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (katikati) akielezea na kumpongeza Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Shear Illusions Bi. Shekha Nasser (aliyeshika zawadi) kwa kulipa kodi stahiki ya Serikali ya kati ya Milioni 9 na 12 kila mwezi kupitia kampuni yake ambayo pia imeweza kutoa ajira kwa vijana zaidi ya12. Pongezi hizo alizitoa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini dar es salaam.
Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka
TRA Bi. Rose Mahendeka alisema kuwa wafanyabiashara wote
ambao wanahitaji kutumia mfumo wa kuuza bidhaa kwa kuweka
msimbomilia (Barcode 620) wanapaswa kupitia TRA kwa ajili ya
usajili na uhakiki wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN)
kabla ya kwenda kupata huduma ya msimbomilia 620.
Bi. Mahendeka aliwasisitiza wadau hao kuhakikisha wanajisajili
na TIN na wale waliojisajili kuhakikisha wanahakiki taarifa zao
ili kurahisisha upatikanaji wa Msimbomilia 620 na kuiwezesha
TRA kupata takwimu sahihi za wafanyabiashara wazalishaji na
wanaouza bidhaa zao nje ya nchi.
Baadhi ya wadau wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa Msimbomilia (Barcode 620) za bidhaa (GS1) wakimsikiliza kwa makini Afisa Mkuu wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Rose Mahendeka akitoa elimu ya kodi wakati wa mkutano wa nne wa mwaka wa Taasisi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
“Wafanyabiashara wote ambao wanahitaji kutumia mfumo wa
kuuza bidhaa kwa kuweka Msimbomilia(Barcode 620) wanapaswa
kupitia TRA kwa ajili ya usajili na uhakiki wa Namba ya
Utambulisho wa Mlipakodi(TIN) kabla ya kwenda kupata
huduma” alisisitiza Bi. Mahendeka.
Aidha Bi. Mahendeka alisema kuwa wafanyabiashara ambao
wanahitaji kuuza bidhaa zao kwa kutumia msimbomilia
wanapaswa kulipa kodi bila ya kukwepa ili kuiwezesha Tanzania
kupiga hatua kufikia uchumi wa viwanda na vilevile kuweza
kutoa huduma bora kwa maendeleo ya jamii.
Naye Mwenyekiti wa bodi ya GS1 Bw. Gideon Mazara alitoa rai
kwa wafanyabiashara wanaozalisha bidhaa kutumia Msimbomilia
620 wa Tanzania na kuweza kutangaza bidhaa za hapa nchini ili
kupata soko la kimataifa litakalowezesha nchi kufikia uchumi wa
kati .
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akiwa katika
picha ya pamoja na baadi ya wadau wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa
msimbomilia (Barcode 620) za bidhaa (GS1) mara baada ya kuhitimisha mkutano
mkuu wanne wa Taasisi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee
jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...