PRIDE (Promotion of Rural
Initiative and Development Enterprise)ni shirika lisilo la kiserikali
(NGO) linalotoa huduma za kifedha kwa masharti nafuu kwa wafanyabiashara
ndogondogo na wa kati. Huduma hizo zina lengo la kuchangia pato la
taifa na kuondoa umasikini nchini.
PRIDE ilisajiliwa mnamo Mei
1993 chini ya wadhamini wasio na hisa (Company Limited by guarantee, not
Having Share Capital) kulingana na Sheria ya Makampuni Cap, 212 ya
mwaka 2012.na kuanza rasmi shughuli zake mwaka 1994 mjini Arusha.Kwa
sasa Shirika lina matawi 85 yalioenea nchi nzima.
Tangu kuanzishwa, PRIDE
imeweza kukopesha wajasiliamali mbalimbali nchini wapatao 1,700,000
nakutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni miatisa (bil. 900.0).
Katika kuungana naWatanzania,
PRIDE Tanzania walitoa misaada mbalimbali moja kwa moja kwa wateja wao
wa tawi la Bukoba ambao waliathirika na tetemeko la ardhi lililotokea
Mkoani Kagera.Msaada huu ulilenga kuwawezesha wateja wa PRIDE kukarabati
makazi yao.
Vilevile PRIDE ilichangia katika mfuko wa maafa wa serikali kwa kutoa mifuko ya saruji na mabati.
Mteja wa PRIDE Tanzania, tawi
la Bukoba, Bw. Revocatus Siliden akionyesha madhara aliyoyapata kwenye
nyumba yake baada ya kutokea tetemeko la ardhi huko Mkoani Kagera.
Afisa wa PRIDE Tanzania,
Ndugu Samson Tenga akimkabidhi Mteja wa PRIDE Tanzania, Tawi la Bukoba
mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba yake ambayo ilibomoka
kutokana na janga la tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera
Brigedia Mstaafu Salum Kijuu akifurahia jambo na mmoja wa wawakilishi wa
wateja wa PRIDE Tanzania, tawi la BukobaBi. Mariam Seleman ambae pia ni
muathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
Diwani wa Kata ya Miembeni,
Manispaa ya Bukoba, Mkoa wa Kagera (Shati la Kijani) Bw. Richard Gaspar
pamoja na maafisa wa PRIDE Tanzania wakimkabidhi mifuko ya saruji mteja
wa PRIDE, ambaye nyumba yake iliathirika na tetemeko la ardhi
lililotokea Bukoba.
Meneja wa Kanda ya Ziwa, Bi.
Hilda Nsombo akikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Mstaafu
SalumKijuu msaada wa mabati na mifuko ya saruji kwa ajili ya waathirika
wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...