Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka sawa mkono wenye drip wa mkewe Mama Janeth Magufuli, ambaye amelazwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu leo Novemba 10, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na mkewe Mama Janeth Magufuli ambaye amelazwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu leo Novemba 10, 2016. Kulia ni Dkt Edward Ngwale akiwa na wauguzi katika wodi hiyo.
: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimjulia hali Waziri wa Zamani Balozi Omar Ramadhani Mapuri ambaye amelazwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu leo Novemba 10, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru na kuwapongeza kwa kazi nzuri baadhi ya madaktari na wauguzi kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alipotembelea wagonjwa pamoja na mkewe ambaye anapatiwa matibabu leo Novemba 10, 2016.
Ajabu kweli kweli! Huyu Mama yeye anatibiwa nchini? Hajapekekwa Ulaya? Mungu Mbariki Magufuli. Mungu Ibariki Tanzania. Tunamuombea Mgonjwa pia.
ReplyDeleteMungu akutie nguvu upone vizuri mama yetu, tunakupenda.
ReplyDeleteThis is leadership by action. Sio wengine wafunge mikanda viongozi ule ule! Tofauti ya matendo ya viongozi na maneno yao ndo yamempatia Bwn Trump ushindi. Huyu Rais amejileta karibu na watu. Ameonyesha uongozi wa kweli. Wacha Wabunge wangang'anie mishahara yao Dodoma wanasaidia kuvijennga vyama vya akina Zitto tu. The should take a leaf from Magufuli's humility.
ReplyDeleteKweli huyu ni raisi wetu anaongoza kwa vitendo.
ReplyDeleteMungu akubariki raisi wetu na nawapa pole wangonjwa wote.