Mshambuliaji wa Timu ya African Lyon Omary Abdallah akiwatoka mabeki wa Timu ya Simba, Novality LUfunga na Jonas Mkude, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja
wa Taifa, Jijini Dar es salaam. African Lyon imeshinda bao 1-0.
Timu
ya African Lyon imefanikiwa kuondoka na alama tatu katika Uwanja wa
Uhuru baada ya kuifunga Simba goli dakika ya 96 na kuweka rekodi ya
kuwafunga wekundu hao wa Msimbazi toka ligi ianze.
African
Lyon waliweza kucheza kwa makini na waliweza kutumiawaliitumia kwenye
kipindi cha kwanza, ilizaa matunda kutokana na kuibana Simba ambayo
ilionekana kushindwa kabisa kupenya safu ya ulinzi ya Lyon.
Pamoja
na kujitahidi kutengeneza nafasi za mabao na kupata kona tatu kwenye
kipindi cha kwanza, mashambulizi mengi ya Simba yaliishia mikononi mwa
kipa Youthe Rostand wa Lyon ambaye alikuwa kikwazo kwenye mchezo huo.
Dakika
nne za nyongeza kwenye mchezo huo, zilikuwa chungu kwa Simba baada ya
mshambuliaji Abdallah Msuhi kuitumia vyema krosi Ya Rahidhan Hafidh na
kuifungia bao Lyon ambalo limevunja rekodi ya Simba kucheza mechi 13 za
ligi bila kupoteza.
Kufungwa
kwa bao hilo kuliwachochea mashabiki wa Simba ambao walianza kurusha
makopo ya maji uwanjani wakionyesha kutoridhishwa na mwamuzi wa pembeni
Frank Komba wakidai kuwa mpigaji wa krosi alikuwa ameotea.
Mshambuliaji
wa Timu ya African Lyon, Abdullah Msuhi akiachia shuti lililoingia moja
kwa moja wavuni na kuiandikia timu yake bao la kuongoza dhidi ya Timu
ya Simba, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya
leo katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. African Lyon imeshinda
bao 1-0.
Mshambuliaji wa Timu ya African Lyon, Abdullah Msuhi akiruka juu kushandilia goli lake dhidi ya Wekundu wa Msimbazi, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya leo katika
Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. African Lyon imeshinda bao 1-0.
Mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo akiichachafya ngome ya African Lyon.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...