Na Dotto Mwaibale
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Angilikana Tanzania, Dk Valentino
Mokiwa amesema migogoro ya kisiasa inayoibuka hivi sasa inaweza kuhatarisha
hali ya amani nchini.
Dk. Mokiwa ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam leo wakati
akiwaongoza waumini wa kanisa hilo Archidikonari ya Kinondoni kutoa
misaada ya vifaa tiba na kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa ya Mwananyamala.
"Migogoro ya kisiasa ambayo imeanza kuzuka hivi sasa
inaweza kuhatarisha amani ya nchi ni vizuri viongozi wanaovutana wakutana na
kuweka mambo sawa" alisema Mokiwa.
Alisema migogoro ya kisiasa inayoendelea inaweza kusababisha
kutoweka kwa amani hivyo ni jukumu la viongozi husika kuliangalia jambo hilo
kwa karibu na kulitafutia ufumbuzi.
Alisema nchi yetu inahitaji amani na utulivu na kuondokana
na matukio ya kuogopesha akitolea mfano miili ya watu saba iliyokutwa ndani ya
viroba vilivyotupwa mto Ruvu Bagamoyo mkoani Pwani.Alisema matukio kama hayo yanaweza kuwafanya wananchi
kukimbia nchi yao kwa hofu hivyo inatakiwa kila mmoja wetu kuwa na hofu ya
mungu.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dk.Valentino Mokiwa (katikati), akiwaongoza waumini wa kanisa hilo Archidikonari ya Kinondoni kufanya usafi katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Dar es Salaam leo asubuhi wakati kanisa hilo lilipotoa msaada wa vitanda na magodoro katika hospitali hiyo vyote vikiwa na thamani ya sh.milioni 12.
Waumini wa kanisa hilo wakiendelea na kufanya usafi.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk.Valentino Mokiwa (kulia), akipanda mti nje ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, wakati alipowaongoza waumini wa kanisa hilo kutoa msaada wa magodoro na vitanda vya wagonjwa pamoja na kufanya usafi wa mazingira Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto anayemsaidia kupanda mti ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk.Daniel Nkungu na wengine ni waumini wa kanisa hilo.
Askofu Dk. Valentino Mokiwa akimkabidhi moja ya kitanda kati ya 15, Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Daniel Nkungu.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...