Rais Mteule wa Gambia, Adama Barrow, ametaja kile alichosema ni
"Gambia Mpya" kufuatia ushindi wake wa kushangaza dhidi ya Yahya
Jammeh, aliyenyakua madaraka mwaka 1994 kwa mtutu wa Bunduki.Bwana Barrow,
aliyekuwa wakati mmoja mfanya biashara wa kujenga na kuuza nyumba ambaye hana
ujuzi wowote wa kisiasa, ameshangazwa na ushindi wake.
Bwana Jammeh amekosolewa na makundi mengi ya haki za kibinadamu kwa
ukiukaji wa haki za raia nchini, alisema kuwa Allah alikuwa akimweleza kuwa
muda wake umekamilika.
Alisema hatapinga matokeo ya uchaguzi na kwamba
ananuia kurudi shambani mwake baada ya kukabidhi madaraka Januari, mwaka ujao.
Maelfu ya wakaazi wa mji mkuu wa Banjul walijitokeza barabarani na kusherehekea matokeo hayo.
Rais Mteule wa Gambia, Adama Barrow akishangilia ushindi.
CHANZO: BBC SWAHILI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...