Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBC) imetangaza kumfungia kwa miaka miwili Bondia wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka kufuatia kitendo chake cha kugoma kupanda ulingoni kuzichapa na Bondia Abdallah Pazi "Dullah Mbabe" pambano lililokuwa lifanyika Desemba 25 mwaka huu, katika Ukumbi wa PTA Saba saba jijini Dar es salaam, lililoandaliwa na Promota Siraju Kaike kupitia kampuni yake ya Kaike Promosion.
Rais wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBC) Chaurembo
Palasa akitoa ufafanuzi zaidi kwa Waandishi wa Habari mapema leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar kuhusiana na sakata la Bondia Francis Cheka,kulia kwake ni Katibu Msaidizi wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBC), Chatta Michael
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Katibu Msaidizi wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBC), Chatta Michael amesema kuwa Kamisheni yake ilitoa kibali cha kufanyika kwa mpambano huo baada ya kujiridhisha kuwa taratibu zote zimefuatwa na mabondia wameridhia na kukubaliana na muandaaji, Ila wameshangwaza na Bondia Francis Cheka kugoma kupanda ulingoni kwa madai ya malipo wakati alishasaini mkataba na muandaaji ulioonyesha kuwa ameshachukua kiasi cha shilingi milioni tatu (3,000,000) na baada ya mpambano alitakiwa kupewa kitita chake cha milioni sita.
Amesema kitendo kilichofanywa na Cheka kinaweza kupoteza uaminifu baina ya mabondia na waandaaji wa mapambano, kujiondoa kwa waandaaji katika mchezo huo kwa kuona hakuna uaminifu na pia kinaweza sababisha uvunjifu wa amani kwa watazamaji, iwapo wataendelea kudanganywa uwepo wa mapambano hewa.
Hivyo Kamati ya utendaji ya Kamisheni hiyo iliyokaa Desemba 27, na kupitia kanuni za mchezo huo, imemkuta Bondia Francis Cheka na makosa ya kimakubaliano na kutangaza kumfungia kujihusisha kwa namna yeyote na mchezo huo na kutakiwa kupipa faini ya shilingi laki tano (500,000).
mmebaki kuwa wababaishaji hakuna maendeleo ya ngumi nchini kazi kuua vipaji, sasa ni nini faida ya kumfungia bondia mkubwa kama Cheka, tatizo viongozi wengi wana inferiority complex tuweke utaratibu wa settlement dispute amicably kwa njia ya makubaliano kwanza tusiinge mifumo ya nje wenzetu wameshapiga hatua za kutosha mabondia kama Cheka wanao zaidi ya 500. nitoe rai kwa viongozi wasiweke maslahi mbele na ubabe uongozi ni tunu ya kufikia katika usuluwishi wa balance of fairness pande zote mbili.
ReplyDelete