Mratibu
wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa
(kulia), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Mheshimiwa Said Mecky
Sadick moja ya kompyuta sita zilizotolewa na taasisi yao kwa mkoa huo
kama msaada wa kuweza kuongeza utendaji kazi mzuri kwa watumishi wa
umma, hususan kwa Manispaa ya Moshi, Halmashauri ya Mwanga na
Halmashauri ya Same, huku kila moja ikipewa kompyuta mbili. Kushoto kwa
RC Sadick ni Katibu Tawala wa Mkoa huo wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Aisha
Amour. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro.
HALMASHAURI
ya Wilaya Same imeanza kupokea faraja za msaada wa kompyuta mbili kati ya sita
zilizofikishwa mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni siku chache baada ya ofisi yao kuungua
moto na kutekeza vifaa mbalimbali vya kiofisi.
Kompyuta
hizo zilipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Said Mecky Sadick,
akiambatana na wakuu wa idara wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na watumishi mbalimbali
kutoka kwenye halmashauri za Same na Mwanga.
Mkuu
wa Mkoa Kilimanjaro, Mheshimiwa Said Mecky Sadick wa pili kutoka
kushoto, akimkabidhi kompyuta hizo alizopokea kwa Taasisi ya Bayport
Financial Services, Katibu Tawala wake wa Mkoa, Mheshimiwa Aisha Amour.
Akizungumza
mwishoni mwa wiki katika hafla ya kupokea kompyuta hizo, Mratibu wa
Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa,
alisema wamekabidhi kompyuta hizo, ikiwa ni siku chache baada ya ofisi
za Halmashauri ya Wilaya ya Same kuungua moto.
Alisema
ingawa msaada wao umekuja kabla ya ofisi hizo kuungua moto, lakini
wanaamini kuwa kompyuta hizo zinaweza kupunguza adha ya watumishi wa
umma kufanya kazi kwa wakati mgumu, huku zikilengwa kwa Halmashauri ya
Same, Mwanga na Manispaa ya Moshi.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Said Mecky Sadick katikati
akizungumza jambo na Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport
Financial Services, Mercy Mgongolwa kulia bada ya kukabidhiana kompyuta
sita za msaada kwa Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Said Mecky Sadick kushoto akimkabidhi kompyuta mwakilishi wa Halmashauri ya Same.
“Taasisi
yetu inatoa pole kubwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na watumishi wote wa
Same, ila tunaamini kwa kiasi kidogo kompyuta tulizotoa zitawafuta machozi
wadau wenzetu wa Same na Serikali yote kwa ujumla hapa nchini,” alisema Mercy.
Naye Mkuu wa
Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Mecky Sadick, aliwashukuru sana Bayport kwa
msaada wao wa kompyuta na kuwataka waendelee kuwasaidia watumishi wa Same kwa
kuongeza idadi ya kompyuta zao.
“Tunapokea
kompyuta hizi kwa mikono miwili lakini tunawaomba wenztu wa Bayport muongeze
idadi ya kompyuta kwa Halmashauri ya Same kwa sababu kule kuna uhitaji mkubwa
zaidi baada ya ofisi kuungua moto.
“Ofisi yetu
imepata pigo kubwa mno hivyo mtusaidie kwa hilo kwa sababu tunafahamu msaada
wenu ni muhimu kwetu na taasisi yenu imekuwa karibu sana na jamii kwa kusaidia
mambo mbalimbali ya kijamii ambayo yana tija kwetu sote,” alisema RC Sadick.
Utaratibu wa
utoaji wa kompyuta 205 kwa ofisi za serikali zenye thamani ya Sh Milioni 500
umeanzishwa ili kuwafanya watumishi wa serikali wafanye kazi zao kwa ufanisi
ili kuhamasisha masuala ya kimaendeleo hapa nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...