Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imemnyima dhamana Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Mhe. Godbless Lema. Mahakama hiyo imeeleza kuwa mawakili wa mtuhumiwa huyo walipaswa kuonesha kusudio la kukata rufaa ndani ya siku 10 kabla ya kukata rufaa.
Hii ni mara ya tano mbunge huyo anakosa dhamana mahakamani tangu alipokamatwa Novemba 3 mwaka huu akiwa mjini Dodoma na kusafirishwa hadi Arusha katika kesi ya uchochezi inayomkabili.
Kesi hiyo itatajwa tena February 2, 2017.
POle Mheshimiwa,lakini ukumbuke ule usemi wa chunga ulimi wako,kwani ungeliweza kutumia busara kuzungumza na ujumbe ungelifika kwa wahusika badala ya haya yaliopelekea leo wateseka na watesa familia yako.Mbona viongozi wenzako wa chama wametulia na wanazungumza kwa hoja.
ReplyDelete