Kamanda wa kikosi cha askari wa usalama barabarani wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Awadhi Haji akiongea na madereva wa daladala mapema asubuhi leo jijini humo baada ya kukamata baadhi yao wakiendesha magari wakiwa wamelewa. ACP Haji amewataka madereva hao na waendesha vyombo vya moto wengine kujiepusha na jinai hiyo ya kuendesha gari wakiwa wamelewa kwani ni hatari kwao binafsi na kwa watumiaji wa barabara. Amesema zoezi hilo la ukaguzi wa madereva wanaofanya kazi wakiwa wamelewa ni endelevu na kwamba atakayepatikana atachukuliwa sheria mara moja bila simile.
Mmoja wa madereva wa daladala akipimwa pumzi kuona kama amelewa ama la. Madereva kadhaa walikutwa wamelewa na kuchukulia hatua.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...