Ripota wa Globu ya Jamii.
Asili ya neno Azonto ni kutoka katika ardhi ya nchi ya Ghana ambapo ngoma ya kplanlongo ilikua ndiyo aina au stepu zake za kiuchezaji, achilia mbali Accra lakini ngoma ya kplanlongo pia huchezwa maeneo ya Tema, Nagua na  Tesha ikiwa ni maeneo ya Pwani ya nchi ya Ghana na hadi kufikia aina ya uchezaji wa kplanlongo uitwe  Azonto kwani ni neno lenye maana ya  msichana wa mtaani ambaye maisha yake sio mazuri kwa hapa kwetu Tanzania unaweza kufananisha na kitorondo na lilianza kutumika miaka ya 1900 kwa kukosoa watu waliokuwa wakipinga kuongezwa kwa shule za wasichana na kuwapeleka wasichana kwenda kusoma hivyo mtindo huo ukatumika katika kampeni za kuhamasisha ujenzi wa shule za wasichana na kuwahimiza umuhimu wa kusoma.

Utamaduni wa mwafrika kupitia makabila ya kibantu ni wa kufanana toka kaskazini hadi kusini na ziko fikra za waafrika wengine zinazo amini kuwa utamaduni wa muziki ni asili ya Afrika na kwamba mzungu aliona zeze akaenda ulaya akaboresha na kuwa gitaa, akaona malimba akaenda akaboresha ikawa kinanda achilia hilo baragumu la pembe akaenda akatengeneza saksafoni .

Afrika ilikua na muziki ila uduni wa vyombo ndiyo ukaweka sura ya kuitwa ngoma za asili,  nchini Ghana kuna makabila mengi kama ilivyokuwa hapa kwetu Tanzania na yanashiriki katika mambo mbalimbali ya kitamaduni kupitia ngoma zao na  miongoni mwa makabila hayo ni kama vile Ashanti, Fante, Akyeni, Kwahu, Ga Ewe, Mamprusi na Dangomba.

Ngoma maarufu za kiasili ni Bamaya Kplanlongo, Klama na Adowa. Sasa Mimi nataka niende na wewe katika kuifahamu hii ngoma ya Kplanlongo ambayo ndo ngoma ya vijana kama ilivyokuw huku kwetu singeli au kiduku maana ilianza kuchezwa pwani kwenye viunga vya jiji la Accra,  Kplanlongo ndiyo yenye mtindo wa kucheza wa Azonto,pia huchezwa katika matukio kama matamasha au mikutano ya kisiasa . 
Uchezaji wake unaegemea katika kuonyesha ishara  za shughuli za kila Siku za mtu kama vile kufua nguo, kupiga pasi nguo,kujiweka sawia  mfano kwa kuchana nywele, kuvaa nguo, kusali, kuendesha  shuguli mbalimbli za michezo kama kuogelea na mengineyo . Baada ya staili hiyo kuibuliwa na kupendwa nchini Ghana  na duniani kote nchi hiyo imeunda  chombo kinachoitwa Azonto Ghana Commission ambacho kazi yake ni kuwatambua wasanii  maarufu wanaotumia staili ya azonto pia kutumika kama idara ya kuinua vikundi vya asili na mtu yoyote mwenye uwezo wa wa kucheza miondoko hiyo na ndicho kinachopewa mamlaka ya kusimamia mkakati mzima wa kutumia staili ya azonto.

Pia idara hiyo inawajibu wa kuitangaza azonto kuwa asili yake ni  Ghana na wachezajj wengi hasa wa Afrika Magjaribi wanapenda kuicheza staili hiyo pale washangiliapo magoli au ushindi wa timu mfano Asamoah Gyan, Emmanuel Adebayor, Mbaraka Wakasso, Emmanuel Ayimang-badu ni kati ya wachezaji wazuri wa wa azonto. Moja kati ya vitu wanavyovipenda waghana ni pale inapotokea mchezo wa soka baina ya Ghana na Togo  bila kujali nani kapoteza kifuatacho ni ushindani wa kucheza azonto baina yao.

Hii ndo ngoma ya Kplanlongo na mtindo wake wa azonto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...