Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan (kushoto)
akimkaribisha Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji
wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kulia) kwenye Ofisi
za Tume zilizoko Posta jijini Dar es salaam. Mhe. Jaji Semistocles
Kaijage ameapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam kuiongoza Tume hiyo
kwa kipindi cha miaka 5.
Baadhi
ya Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakimpokea Mwenyekiti
mpya wa Tume hiyo mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Tume ya Taifa
ya Uchaguzi Posta, jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti
mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe.
Jaji Semistocles Kaijage (kulia) akiwa Ofisini kwake kwa mara ya kwanza
mara baada ya kuapishwa leo. Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameteuliwa
kuongoza Tume hiyo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia tarehe 20
Desemba, 2016.
Mwenyekiti
mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe.
Jaji Semistocles Kaijage (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi ofisini kwake leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...