Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amezitaka Kampuni za
Mawasiliano kukamilisha taratibu za usajili katika Soko la Hisa la Dar es
Salaam kwa kuuza asilimia 25 ya hisa zote kadri ya Sheria ya Masoko ya Mitaji
na Dhamana inavyoelekeza mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar
es Salaam, Prof. Mbarawa ametaja kampuni hizo kuwa ni zile zenye leseni za
mawasiliano zilizotolewa kabla ya tarehe 1 Julai 2016 kwa ajili ya Miundombinu
ya Mawasiliano, Huduma za Mawasiliano, na Huduma za Matumizi.
“Watoa huduma wote wa
Mawasiliano wajisajili na kuuza hisa zao kwa wananchi ndani ya mwezi wa
Disemba”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Ameongeza kuwa kwa Kampuni
zilizopata leseni baada ya tarehe mosi Julai, 2016 watatakiwa kutimiza sharti
hilo la kisheria kwa kipindi kisichozidi miaka miwili tangu kusajiliwa.
Waziri Prof. Mbarawa
amesisitiza kuwa Kampuni zitakazokiuka Sheria hiyo zitachukuliwa hatua za kisheria
kupitia kifungu cha 21 (C) cha EPOCA, 2010.
Aidha, amewataka
wananchi kutumia fursa hiyo kununua hisa hizo na kuwa sehemu ya wamiliki wa
makampuni ya Mawasiliano ili kuongeza kipato na kushiriki katika maamuzi ya
kampuni hizo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu utekelezaji wa sheria ya EPOCA kulingana na mabadiliko yaliyofanywa katika Sheria ya Fedha No. 2 ya mwaka 2016, jijni Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...