Na Mathias Canal
Mwili wa Aliyekuwa
Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi (SACP) EX Peter Kakamba umeagwa na wamia ya wakazi wa Mkoa wa Singida wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Methew Mtigumwe.
Kakamba alifariki dunia alfajiri ya tarehe
30/11/2016 katika hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa
matibabu.
Kakamba
alizaliwa mwaka 1963 katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda, mkoa
wa Katavi. Alisoma shule ya msingi Shanwe Kawajense mwaka 1973 hadi
1980, Kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari
Kantalamba mwaka 1981 hadi 1984 ambapo kidato cha tano na sita alisoma
katika shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro mwaka 1985 hadi 1987.
Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma Astashahada ya Sheria katika Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
Marehemu
alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake
alipandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti
wa Polisi (1991), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi
(2003), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008),
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2011), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2015)
na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2016).
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba ukitolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya VETA mjini hapa kwa ajili ya kuagwa na viongozi mbalimbali na wananchi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe. Baada ya kuagwa kwa mwili huo umesafirishwa hadi kijiji cha Kawajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi.
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba ukitolewa kwenye basi dogo lililobeba mwili huo kutoka hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar-es-salaam. Mwili huo umefikishwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi mjini Singida kwa ajili ya kuagwa leo (01/12/2016).
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akiwashukuru wananchi waliojitokeza kwa wigni kuungana na familia kwa ajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba, Dkt Lutambi amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iko pamoja na wafiwa na watashiriki mazishi kijiji cha Kowajese Mkoani wa Katavi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Mayalla Towo akiwashukuru wananchi, taasisi na mashirika mbalimbali walioshiriki msiba huo, Towo amesema marehemu alikuwa kiongozi bora aliyependa kuwafundisha na kuwaelekeza ujuzi na maarifa aliyonayo watumishi walio chini yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...