Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Bw. Buhacha Baltazar Kichinda ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya utawala na rasilimali watu akiwaaga Vijana 43 wanaojiunga na kambi ya JKT Makutopora kikosi cha KJ 834 kwa hiyari kwa mkataba wa miaka ya miwili. Bw. Kichinda amesema wakiwa jeshini watafundishwa uzalendo, ukakamavu, stadi za jamii na nidhamu. Pia amewaasa wazazi kuwapeleka shule watoto wao  na kupokea fursa kama za jeshi.
Kulia ni Afisa Tawala ofisi ya Mshauri wa Mgambo Meja Rhinocerus Magembesoni 

 Vijana 43 wa Kihadzabe wakipanda mabasi kuelekea katika kambi ya JKT Makutopora kikosi cha KJ 834 kujiunga na kikosi hicho kwa hiyari kwa mkataba wa miaka ya miwili mara baada ya kuagwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida. Jamii ya kihadzabe huendesha maisha yao kwa kuwinda na kula nyama pori, matunda ya porini, asali na mizizi.
 Mmoja wa kijana wa kihadzabe Zuhura Ramadhani Longa ambaye alikuwa akiwasindikiza vijana wenzake kuwinda na kurina asali, amesema ameamua kujiunga na jeshi ili aweze kuisaidia familia yake lakini pia aweze kulitumikia Taifa.
 Vijana 43 wa Kihadzabe wakipunga mikono kuonyesha utayari wa kujiunga na kambi ya JKT Makutopora kikosi cha KJ 834 kwa hiyari kwa mkataba wa miaka ya miwili mara baada ya kuagwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida. Jamii ya kihadzabe huendesha maisha yao kwa kuwinda na kula nyama pori, matunda ya porini, asali na mizizi.
Vijana wa Kihadzabe ambao walikuwa wanawinda na kurina asali, wamesema wameamua kujiunga na jeshi ili waweze kusaidia familia zao na pia kulitumikia Taifa. Picha na Ofisi ya RC Singida

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...