Ujumbe wa Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete kufuatia tukio la kinyama lilimtokea Ndugu Augustino Mtitu mkulima wa kitongoji cha Upangwani, Kijiji cha Dodoma Isanga, Kata Ya Masanze Jimbo la Mikumi la kuchomwa mkuki mdomoni. ujumbe huo unaanzia hapa, Kwanza niruhusu nikupe Pole ndg yangu kwa lililokukuta. La msingi Serikali inatakiwa kujua, tunaposema na kutoa maoni yetu pale Bungeni tunamaanisha. yako mambo unaweza yafanyia utani lakini hapa tulipofika si kwa kuchukulia mzahamzaha.
Waziri muhusika haya hauyaoni au niliposimulia juu ya Wananchi wa Jimbo la Chalinze kupigwa, kuvunjwa migongo na mwengine kupigwa mshale wa goti na kumpa Ulemavu wa Maisha mlizani natania. Sasa hili liwe fundisho. Serikali ni lazima ije na majibu sahihi juu ya kunusuru vita ya wenyewe kwa wenyewe .
Jana mtu kavunjwa mgongo, mwengine mlemavu leo kapigwa mkuki wa mdomo umetokea shingoni. Lini tutasikia kilio hiki. Serikali sikieni kabla Damu ya Watanzania wanyonge wanaotegemea kilimo kama kiinua mgongo chao hawajapotea. Kuna sheria na mipango ya matumizi bora ya Ardhi. nini kinafichwa?
Binafsi Nalaani Vitendo hivi na kuiasa Serikali yangu kujipanga vizuri kabla mambo hayajaharibika. yalianza Kilosa, Mvomelo, Chalinze, Handeni, Kiteto na sasa Mikumi (kutaja maeneo machache). Serikali jipangeni, kabla hapajachafuka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...