Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation,Sandra Oswald akimkabidhi moja ya msaada Godfery Mkukuta ambaye ni mlemavu anayelelewa katika kituo cha kulelea watoto walemavu cha Siuyu Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.Msaada huo wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15/- Msaada huo umetolewa na Vodacom Tanzania Foundation,kulia ni msimamizi wa kituo hicho Padri Tom Ray Sac.
Meneja ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation,Sandra Oswald(kulia)akimsukuma Said Ally kwenye baiskeli yake ambaye ni mlemavu anayelelewa katika kituo cha kulelea watoto walemavu cha Siuyu Wilaya ya Ikungi mkoani Singida,alipofika kituoni hapo kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 15/- kwa niaba ya Vodacom Tanzania Foundation.
Said Ally ambaye ni mlemavu anayelelewa katika kituo cha kulelea watoto walemavu cha Siuyu Wilaya ya Ikungi mkoani Singida(kushoto)akipokea blanketi kwa niaba ya watoto wenzake wa kituo hicho toka kwa Meneja ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation,Sandra Oswald,alipofika kituoni hapo kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali wenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 15/-kwa niaba ya Vodacom Tanzania Foundation.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...